Na Faraja Gasto
Nakusalimu katika jina la Yesu.
Leo ikiwa ni sehemu ya kwanza ya somo hili ningependa kuanza na utangulizi.
Kuweka vipaumbele (priorities) ni suala la kiroho kabisa kwa kuwa hata Mungu huwa anaweka vipaumbele na pia shetani naye huwa anaweka vipaumbele.
KUWEKA VIPAUMBELE MAANA YAKE NINI?
Ni utaratibu wa kuamua kipi uanze kufanya na kipi kifuatie baada ya hicho, hiyo ndio maana rahisi ya kuweka vipaumbele.
(Mwanzo 1:1)
Kabla Mungu hajaanza kuumba chochote alianza kwanza kuweka vipaumbele kumbuka uumbaji ulikuwa mpango(plan) ndio maana utaona alipoanza kuumba alianza na "mbingu na nchi" kwa hiyo vipaumbele vya Mungu vilikuwa ni mbingu na nchi.
MWANZO WA SOMO
NAMNA YA KUWEKA VIPAUMBELE
(1).Kuweka vipaumbele kwa kuzingatia UMUHIMU wa jambo.
(Mwanzo 1:1)
Mungu alipoona amepanga kuumba vitu vingi ambavyo vitaitegemea mbingu na nchi, alianza kuumba mbingu na nchi kwa sababu hivyo ndivyo vilivyokuwa na umuhimu mkubwa kuliko vingine.
Unaweza ukajiuliza kwa nini aanze na mbingu na nchi?
a.mwanadamu alitakiwa aumbwe kutoka kwenye nchi(ardhi).
b.Mungu alikusudia kumpa mwanadamu jukumu la kuilima ardhi.
c.Mungu alikusudia mbingu zitoe mvua kwa ajili ya nchi.
d.Wanyama walitakiwa wakae usoni pa nchi.
e.Mwanadamu asingepata chakula kama nchi isingekuwepo.
N.K N.K
Hizo ni sababu chache kwa nini vipaumbele vya Mungu vilikuwa mbingu na nchi.
Ni vema uelewe kuwa unapokuwa na malengo lazima ujifunze kutumia kanuni hii ya kiungu(divine principle) ili uweze kutimiza malengo yako, ni muhimu ukajiwekea vipaumbele vyako kabla ya kufanya jambo lolote.
Mungu akubariki tukutane wakati mwingine.
©Faraja Gasto
The Mission Man.
0 Maoni