Na Faraja Gasto
Katika sehemu ya kwanza nilikuonyesha jinsi Mungu alivyojiwekea vipaumbele kabla hajaanza kuumba, nilikuonyesha namna ya kuweka vipaumbele kwa kuzingatia umuhimu wa kitu, yaani kipi kianze na kipi kifuatie kutegemeana na umuhimu wa kitu.
NAMNA YA KUWEKA VIPAUMBELE
(2)Lazima uweke vipaumbele kwa kuzingatia UWEZO WAKO
Ninapozungumzia uwezo wako namaanisha uwezo wako wa kufanya(your capability of doing something) na pia uwezo wa kifedha au kiuchumi(financial muscles)
KWA MFANO:Jaribu kufikiri unahitaji kufanya biashara lakini uwezo wako wa kifedha ni mdogo yaani hauna mtaji ni wazi kabisa hiyo biashara hautaweza kuifanya, na pia kama utafanya biashara ambayo hauna uwezo nayo ni wazi kabisa itakushinda, kwa mfano jaribu kufikiri unataka kufanya biashara ya kufuga kuku wa mayai lakini kwa wakati huo hauna uwezo nayo, hauna ufahamu juu ya namna ya kufanya hiyo kazi ni wazi kabisa hayo malengo ya biashara hayatatimia.
KOSA AMBALO WATU WENGI WANALIFANYA NI KUTAKA KUFANYA MAMBO AMBAYO HAYAKO NDANI YA UWEZO WAO NA MWISHO WA SIKU MALENGO YA WATU WA NAMNA HIYO HUWA HAYATIMII.
Ukitaka kutimiza malengo yako lazima vipaumbele vyako vizingatie uwezo wako, yaani unapotaka kufanya jambo anza kwanza kwa kutazama uwezo wako.
(1 Mambo ya Nyakati 29:1-3)
Mfalme Daudi alitamani sana kujenga hekalu(hilo lilikuwa lengo lake) lakini Mungu alimzuia asijenge yeye bali ajenge mwanae Sulemani.
Baada ya hapo Mfalme Daudi ALITAZAMA UWEZO WAKE akaona uwezo wake ni mdogo ukilinganisha na kazi aliyotaka ifanyike(ujenzi wa hekalu) kwa hiyo Mfalme Daudi alianza kuweka AKIBA, kuweka akiba ndicho kilikuwa kipaumbele cha Mfalme Daudi, akiba ziliwekwa ili zije zimsaidie Sulemani kujenga hekalu la Bwana.
MAMBO TUNAYOJIFUNZA HAPO
(a)Unapokuwa na malengo makubwa huku uwezo wako ni mdogo lazima ujifunze kujiwekea akiba.
(b)Usije ukaanza kufanya jambo lolote kabla ya kutathimini kiwango cha uwezo wako wa kufanya vitu na uwezo wako wa kiuchumi.
Mungu akubariki, tukutane wakati mwingine.
Faraja Gasto
The Mission Man
0 Maoni