HAKIMU hawezi kutoa hukumu akiwa nyumbani kwake, hukumu inaweza kutolewa katika eneo rasmi la mahakama au mahali palipoidhinishwa kwa mujibu wa sheria ili kulinda haki ya mshitaki na mshitakiwa kusikilizwa na kutendewa haki.
Ninachotaka nikufundishe ni kwamba, KUNA NAMNA MAMLAKA ZINATENDA KAZI KUTEGEMEANA NA NAFASI.
Jambo mojawapo linaloifanya mamlaka itende kazi ni NAFASI AU MWENYE MAMLAKA KUWA KWENYE NAFASI YAKE.
Kuna mamlaka haziwezi kutenda kazi nje ya nafasi au ikiwa mwenye mamlaka hiyo hayuko kwenye nafasi.
👉Ukitoka kwenye nafasi ambayo Mungu amekuweka, mamlaka aliyokupa Mungu haiwezi kutenda kazi.
👉KAA KWENYE NAFASI yako ili mamlaka ambayo Mungu amekupa zitende kazi.

0 Maoni