UTANGULIZI
Mjane ni mtu aliyefiwa na mumewe, rejea kitabu cha Kutoka 22:22, Kumbukumbu la torati 16:11, Kumbukumbu la torati 27:19, 2 Samweli 14:5).
Biblia inatambua wanawake walioachwa na waume zao na walioachishwa waume lakini haiwaiti wanawake hawa kuwa ni wajane, wanaitwa hivyohivyo wanawake walioachwa na waume zao na wanawake walioachishwa waume, rejea (Mambo ya walawi 22:13)(Hesabu 30:9).
Mjane anaweza kuwa mwanamke kijana au mzee maadamu amefiwa na mume wake, huyo anaitwa mjane, rejea kitabu cha 1 Timotheo 5:11 & 14.
AINA ZA WAJANE KWA MUJIBU WA BIBLIA
1. Wajane kwelikweli - wazee (1 Timotheo 5:3-5)
Hawa ni wajane ambao hawana watu wa kuwasaidia, hawana vitega uchumi vya kuwasaidia pia wamekuwa na mume mmoja yaani mjane hajawahi kuwa na mume mwingine isipokuwa mume wake aliyefariki pia ana miaka kuanzia sitini (1 Timotheo 5:9)
2. Wajane vijana
Hawa ni wajane vijana pia wana watu wa kuwasaidia.
MAMBO BAADHI YANAYOWAKABILI WAJANE
1. Kuteswa (Kutoka 22:22) kama Mungu alizuia wajane wasiteswe inadhihirisha kuwa wajane walikuwa wanateswa.
2. Kupokonywa, kunyimwa na kudhulumiwa haki zao (Luka 18:2-5)(Luka 20:47)
3. Kuonewa (Ezekieli 22:7)(Kumbukumbu la torati 24:17).
4. Umasikini (Kumbukumbu la torati 24:19-20).
WAJANE WANAHITAJI NINI?
1.Kutetewa (Isaya 1:17).
2.Kupewa haki zao (Luka 18:2-5).
3.Kusaidiwa mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile mavazi, chakula na malazi (Kumbukumbu la torati 24:19-20).
NANI ANAWAJIBIKA KUWAHUDUMIA WAJANE?
Kanisa linawajibika kuwahudumia wajane (1 Timotheo 5:16)(Matendo ya mitume 6:1-3)
Mitume walikuwa na utaratibu wa kuwahudumia wajane, kwa kuwa tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii lazima kanisa lihudumie wajane.
Katika kuwahudumia wajane, Biblia inasema wajane waandikwe orodha yao wale wenye miaka sitini na kuendelea (1 Timotheo 5:9,11).
Wahusika wa mjane (1 Timotheo 5:4,16).
Wahusika wa mjane wanaweza kuwa watoto wa mjane au watu wake wa karibu wanapaswa kumsaidia ili kanisa lisilemewe na mzigo wa kuhudumia yatima.
Watu binafsi ambao wamejitolea kuwasaidia wajane (Matendo ya mitume 9:36-39).
Biblia inaeleza kuhusu mwanamke mmoja aliyeitwa Dorcas, huyu mwanamke alijitolea kuwasaidia wajane mavazi.
(Ayubu 29:13) Ayubu alijitolea kuwasaidia wajane.
HITIMISHO
Biblia imetoa mwongozo kuhusu mambo yahusuyo wajane kama ambavyo tumeona hapo juu, Biblia imetoa maelekezo kwamba wajane wasaidiwe pia wajane ambao ni vijana waolewe ili wawe na madaraka ya nyumbani (1 Timotheo 5:14).

0 Maoni