KUHUSU UANAUME


 

Yaani ni wanaume kwa jinsi ya nje lakini ndani ni WANAWAKE.

USISHTUKE

Tuanzie hapa kwenye kipande cha maneno yaliyokuwa kwenye wosia wa Mfalme Daudi kwa mwanaye Sulemani (Mfalme Sulemani) kuna jambo kubwa la kujifunza hapa. Rejea kitabu cha kwanza cha Wafalme sura ya pili msitari wa pili (2 Wafalme 2:2).

KSWAHILI CHA KIMVITA 

1 Wafalme 2:2. Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, UKAJIONYSHE KUWA MWANAMUME.

Soma Biblia hizi za kingereza zilivyoeleza neno hilo "UKAJIONYESHE KUWA MWANAMUME"

NEW KING JAMES VERSION

"I go the way of all the earth; be strong, therefore, and PROVE YOURSELF A MAN.

Kwa kiswahili kisicho rasmi anasema "THIBITISHA KWAMBA WEWE NI MWANAMUME" maana yake ni kwamba kuna mambo yakifanywa huthibitisha huyu ni mwanamume halisi, unaweza kuthibitisha uanaume wako kupitia utendaji wako au namna unavyofanya mambo.

NEW LIVING TRANSLATION

“I am going where everyone on earth must someday go. Take courage and BE A MAN.

Kwa kiswahili kisicho rasmi anasema "KUWA MWANAMUME" unaweza kushangaa anaambiwaje awe mwanamume wakati yeye ni mwanamume tayari? jibu rahisi ni kwamba KUWA NA JINSIA YA KIUME HAIMAANISHI WEWE NI MWANAMUME.

AMPLIFIED BIBLE

 I go the way of all the earth. Be strong and SHOW YOURSELF A MAN.

Kwa kiswahili kisicho rasmi anasema "JIONYESHE KUWA MWANAMUME" yaani dhihirisha kama wewe ni mwanamume kweli, dhihirisha uanaume wako.

NEW INTERNATIONAL VERSION

“I am about to go the way of all the earth,” he said. “So be strong, ACT LIKE A MAN.

Kwa kiswahili kisicho rasmi anasema "TENDA KAMA WANAUME" yaani kuna namna wanaume hufanya mambo yao au kuna namna wanaume hutenda mambo yao, namna wanavyotenda hudhihirisha huyu ni mwanamume. 

MFALME DAUDI ALITAKA MWANAYE AFAHAMU NINI KWA KAULI HIYO?

1. Uanaume uko ndani ila jinsia ya kiume iko nje.

2. Uanaume ni utendaji sio jinsia ya kiume, yaani namna mtu anavyotenda au anavyofanya mambo hudhihirisha kuwa yeye ni mwanamume halisi au sio mwanamume. Mwanamume halisi hutambulika kwa vile anavyotenda au anavyofanya mambo.

3. Mwanamume anapaswa kudhihirisha uanaume wake kupitia utendaji wake au mambo anayofanya.

4. Kuna mambo hayawezi kwenda kama mwanamume hajasimama kama mwanamume.

👉WEWE NI MWANAMUME AU UNA JINSIA YA KIUME?

Chapisha Maoni

0 Maoni