Tangu zamani watu wengi wamekuwa wanatafuta upendeleo wa watawala (kufurahiwa na kupendwa na watawala), kwa kuwa upendeleo wa mtawala ni fursa kubwa sana.
Mtawala akikupenda au akikufurahia anaweza kukufanya kuwa msaidizi wake, anaweza kukupa vitu, mambo yako yatafanikiwa kwa wepesi sana, unaweza kujikuta umepandishwa cheo nakadhalika NDIO MAANA WATU HUTAFUTA UPENDELEO WA MTAWALA.
Jitihada za kupendwa na watawala ndizo ambazo huzaa watu ambao kwa kiswahili cha sikuhizi wanaitwa MACHAWA (machawa wamekuwepo tangu zamani).
Mbinu mojawapo inayotumiwa na watu wengi kupata upendeleo wa watawala ni KUJIPENDEKEZA KWA MTAWALA AU KWA WATAWALA.
Mbinu mojawapo inayotumiwa na wanaojipendekeza kwa mtawala ni KUMSIFIA AU KUMSIFU MTAWALA HATA AKIFANYA JAMBO AMBALO SIO SAHIHI (watawala nao ni wanadamu huwa wanafanya makosa).
Mtawala asipokuwa makini kuwabaini watu wanaompenda kweli na wale wanaojipendekeza kwake anaweza kujikuta amezungukwa na maadui zake wa sirini au maadui zake wa siku za usoni, ili mtawala awe salama anapaswa kuhakikisha anakaa mbali na wanaojipendekeza kwake kwa kuwa watu hao ni hatari kwake.
Dalili zinazoonyesha mtawala amezungukwa na watu wabaya au wanaojipendekeza (1)ni pale ambapo mtawala anafanya makosa fulani halafu waliomzunguka hakuna hata mmoja anayemwambia "mkuu umekosea" (2) pale ambapo siri zinavujishwa, mtawala anapanga jambo lakini mtu wake au watu wake wanavujisha siri.
0 Maoni