KWA WATUMISHI WA MUNGU VIJANA


Nimewaandiki enyi watumishi wa Mungu vijana ingawa nilichoandika kinaweza kuwasaidia watumishi wa Mungu wengine ambao sio vijana ila kwa wakati huu nimewaandikia enyi watumishi wa Mungu vijana.

✍️✍️✍️

Shetani haoni hasara kukufungulia milango mbalimbali ikiwemo ya kulala na wanawake (milango ya uzinzi au uasherati) haoni hasara kukufungulia milango ya kiuchumi inayokutoa kwenye kusudi la Mungu, haoni hasara kukufungulia milango ya fursa ya aina yoyote ili kukutoa kwenye kusudi la Mungu.

Shetani alimwambia Yesu "ukinisujudia nitakupa milki zote za ulimwengu" (Mathayo 4:8-9) hii ilikuwa fursa ya kiuchumi na kiutawala.

Unamkumbuka Yusufu mtoto wa Yakobo aliyekuwa anafanya kazi kwa Potifa, mara paaaaaaap fursa hiyo hapo, mke wa Potifa akamtamani bwana mdogo, akamwambia LALA NAMI TU (Mwanzo 39:7).

Ninachoamini mke wa Potifa alimuahidi Yusufu mambo mengi kwamba ukilala na mimi nitakufanyia au nitakupatia 1,2,3,4.............. Kama shetani alivyomwambia Yesu ukinisujudia nitakupa milki zote za ulimwengu.

LAKINI Yusufu naye aligoma kulala na na ule mshangazi kama ambavyo vijana mnawaita wanawake wakubwa kiumri, kama Yesu alivyogoma kumsujidia shetani.

IKO HIVI

Sio Mungu tu anayefunguaga milango mbalimbali kwa watumishi wake hata shetani huwafungulia milango ya fursa mbalimbali watumishi wa Mungu ili awatoe kwenye kusudi la Mungu.

Uwe macho kuchunguza kila fursa inayokuja kwako, FURSA ZINGINE ZINALETWAGA NA SHETANI ILI AKUKAMATE.

Ulichobeba ndani yako (kusudi la Mungu, unadhiri, ndoto ya Mungu aliyokuonyesha kama Yusufu nakadhalika NI YA MUHIMU SANA KULIKO MALI NA VINGINE, HAKIKISHA UNASIMAMA IMARA).

Chapisha Maoni

0 Maoni