Bwana Yesu asifiwe sana, ikiwa ni sehemu ya nne ya somo hili napenda nikuonyeshe njia ya nne ambayo Mungu anaitumia
4. Mungu Huwa Anatumia WASIWASI,
Hali ya wasiwasi huwa inaachiliwa moyoni mwa
mtu ili kumfanya mtu asipite njia Fulani, au asiende mahali Fulani n.k
Nadhani hii hali imewahi kukupata wewe au
umeshawahi kusikia mtu akisema “nataka
kwenda sehemu Fulani lakini moyo wangu unakataa kabisa” au mtu anasema
“nimepanga kwenda sehemu Fulani lakini moyo wangu umekuwa na wasiwasi”.
Watu wengi huwa hawaelewi sana maana ya
WASIWASI huo wanaopata wanapotaka kupita njia Fulani au kwenda sehemu, wengine
hudhani ni hali ya kawaida tu kumbe hiyo ni taarifa Mungu anawapa kuhusu hatari
au shambulizi lililoko mbele endapo watapita njia Fulani au watakwenda huko
wanakotaka kwenda, ndio maana utaona mtu akipuuzia hiyo hali na ikatokea
amekwenda huko au amepita njia Fulani utakuta yanampata mambo mabaya halafu
anasema “ndio maana nilipata wasiwasi kusafiri au kupita hii njia”
Hayo yanatokea kwa kuwa wengi wanapuuzia
taarifa wanayopewa na Mungu, taarifa iliyokuja kwa ishara ya wasiwasi moyoni
mwa mtu.
Hebu tujifunze kuhusu Mtumishi wa Mungu Paulo
jinsi alivyoiona HATARI iliyokuwa mbele yao katika kipindi walichokuwa
safarini.
(Matendo ya mitume 27:9-21)
Huo ni wakati Paulo alipokuwa akisafirishwa
kwenda mahali Fulani kwa masuala ya kesi iliyokuwa inamkabili, lakini ghafla
Paulo alijikuta akiwa na WASIWASI kuhusu hiyo safari, wasiwasi uliingia moyoni
mwake na akaelewa maana yake ni nini, ndipo akawaambia kuwa “hiyo safari
itakuwa na madhara makubwa kama wataamua kusafiri” lakini kwa kuwa alikuwa
mtuhumiwa hawakumsikiliza mwishowe walipata hasara kubwa sana kwa kuwa
walipuuzia taarifa waliyopewa kuhusu hatari iliyokuwa mbele yao.
JIULIZE: Mara ngapi Mungu ametumia ishara hii
kukutahadharisha halafu ukapuuzia?
Kama ulipuuzia najua uliona madhara yake, kwa
hiyo ni muhimu kuwa makini sana ili usije ukapatwa mambo mabaya na ukamlaumu
Mungu kumbe shida ni yako mwenyewe.
Japo nimeeleza kwa uchache, unaweza ukasoma
Biblia ukajifunza zaidi kuhusu hizo njia mbazo Mungu anazitumia kukupa taarifa
kwa ajili ya usalama wako.
Mungu akubariki sana kwa kufuatilia somo hili
mwanzo mpaka mwisho.
Mwl.Faraja Gasto
+255767955334
0 Maoni