Kwa mfano fedha ni ya thamani kwa kuwa ni kitu ambacho kinahitajika kwenye maisha ya kila siku.
Ukitaka kuwa wa thamani hakikisha unakuwa mtu unayehitajika (mtu ambaye watu wanamuhitaji).
WATU WANAHITAJI WATU WA AINA GANI?
Hawa ni baadhi ya aina ya watu ambao watu wanawahitaji, hata wewe unawahitaji watu wa aina hii
1. Watu wenye masuluhisho ya matatizo ya watu wengine.
2. Watu wanaoweza kuwasaidia wengine kupenya mahali fulani au kufika mahali fulani.
3. Watu wenye ujuzi au mawazo yanayochangia ukuaji, maendeleo na ufanisi wa taasisi au jambo fulani.
UNAWEZAJE KUWA MTU AMBAYE WATU WANAKUHITAJI
Haya ni mambo baadhi yatakayokufanya kuwa mtu ambaye watu wanakuhitaji,
1. Beba nguvu za Mungu zinazoweza kuwasaidia watu katika maisha yao.
Nguvu za Mungu ni jambo pana sana, ni jambo pana kwa kuwa nguvu za Mungu sio kitu kimoja ziko aina nyingi sana za Mungu za Mungu kwa mfano nguvu za Mungu ni pamoja na maarifa ya kiungu, hekima ya kiungu, mamlaka ya kuamuru mambo na yakatokea nakadhalika.
Watu wanahitaji mtu mwenye nguvu za Mungu awasaidie kuwaondolea pepo wanaowatesa na kuwafungua kutoka kwenye minyororo ya shetani, kuwaondolea mikosi na laana zinazowatesa, kuwasaidia kutoka kwenye mikwamo mbalimbali ya kimaisha, kimaamuzi nakadhalika.
2. Uwe na maarifa ambayo watu hawana na wanayahitaji.
Kwa mfano wakati Mfalme Sulemani anataka kujenga hekalu, alihitaji watu wanaojua kukata na kuchonga miti ifaayo kwa ujenzi wa hekalu, watu wa aina hiyo hawakuwepo kwenye taifa lake ilibidi akaazime au akakodi watu hao kwenye taifa lingine (soma 1 Wafalme 5:2-6).
Bila shaka thamani ya watu hao ilikuwa kubwa sana kwenye taifa la Mfalme Sulemani kwa kuwa wao pekee ndio walikuwa wana ujuzi kuhusu masuala ya miti.
3. Weza ambacho wengine hawawezi.
Kama kuna ambacho wengine hawawezi, ukikiweza lazima utakuwa mtu ambaye wanakuhitaji sana.
Ukiwa na maarifa ambayo watu hawana na wanayahitaji, uwe na uhakika utakuwa mtu unayehitajika sana kwa watu hao.
👉Kila mara hakikisha wewe ndiye mtu ambaye watu wanakuhitaji.

0 Maoni