Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli aliwaua wagibeoni, Gibeoni ulikuwa ni mji mmojawapo wa wahivi (Yoshua 9:17), hao watu aliowaua Mfalme Sauli walikuwa wakazi wa mji huo wa Gibeoni.
Kitendo cha Mfalme Sauli kuwaua wagibeoni kilikuwa ni kosa mojawapo alilofanya kwa kuwa kulikuwa na agano (mkataba) kwamba Waisraeli hawatawaua wagibeoni, agano hilo (mkataba huo) ulifanywa wakati Yoshua alipokuwa kiongozi wa taifa la Israeli, rejea kitabu cha Yoshua sura ya tisa (Yoshua 9).
MADHARA YA MAUAJI HAYO hayakuathiri nyumba ya Mfalme Sauli tu bali yaliathiri utawala wake pia yaliathiri utawala wa Mfalme Daudi (Mfalme aliyefuata baada ya Mfalme Sauli), biblia inatujulisha kuwa wakati wa utawala wa Mfalme Daudi kulikuwa na njaa kwa muda wa miaka mitatu, nchi ilikuwa katika hali mbaya, kulikuwa na shida kuhusu masuala ya chakula (food insecurity) na mengineyo yanayozaliwa na njaa.
Kama Mfalme Daudi asingemtafuta Mungu nina hakika lile tatizo la njaa lisingepata ufumbuzi, nchi ingeendelea kuwa na hali mbaya ya masuala ya chakula na mengineyo yanayozaliwa na njaa.
DAMU NA MASUALA YA KITAIFA NA UTAWALA
1. Mtawala akimwaga damu za watu anaathiri utawala wake na tawala zitakazofuata kwa kuwa MTU ANAWEZA KUFA LAKINI DAMU HUWA HAIFI ITAENDELEA KULALAMIKA NA KUWA NA MADAI MBALIMBALI, rejea kitabu cha Mwanzo sura ya nne msitari wa tisa na kumi (Mwanzo 4:9-10).
2. Tatizo la njaa lililotokea kwenye utawala wa Mfalme Daudi lilitengenezwa na Mfalme Sauli aliyemwaga damu za watu ambao hakupaswa kuwaua, KWA HIYO MAKOSA YA MTAWALA MMOJA YANAWEZA KUATHIRI TAWALA ZITAKAZOFUATA.
3. Mfalme Daudi alipomtafuta Mungu, Mungu alimwambia chanzo cha tatizo la njaa kwenye nchi ambalo limetokea kwenye utawala wake, KUMTAFUTA MUNGU NI MBINU MOJAWAPO YA KUWASAIDIA WATAWALA KUJUA NAMNA YA KUKABILIANA NA MATATIZO YANAYOTOKEA KWENYE NCHI ZAO WAKATI WA TAWALA ZAO.
4. Watu wakiuawa kinachokufa ni miili ila DAMU HAZIFI, damu zikimwagwa huwa zinakuwa na malalamiko na madai mbalimbali, kuna mbinu mbalimbali za KUNYAMAZISHA DAMU HIZO ILI ZISIENDELEE KUWA NA MALALAMIKO NA MADAI, ashukuriwe Mungu mbinu za kushughulikia damu za watu waliouawa katika zama hizi za agano jipya NI MBINU BORA ZAIDI YA ZILE MBINU ZA ZAMANI.
Mbinu iliyotumika kunyamazisha damu za wagibeoni waliouawa na Mfalme Sauli ilikuwa kuwafuata wagibeoni na kusikiliza walichotaka, walichotaka ni kupewa watu saba wa nyumba ya Mfalme Sauli ili wawaue (kisasi), Mfalme Daudi alikubali matakwa ya wagibeoni, SISI TUNAOISHI KATIKA ZAMA HIZI ZA AGANO JIPYA HATUWEZI KULIPIZA KISASI, KISASI NI JUU YA BWANA (Warumi 12:17-21), Zipo mbinu za kibiblia za agano jipya za kunyamazisha damu za waliouawa.
HITIMISHO
Tuepuke kumwaga damu za watu kwa ajili ya utawala bora.

0 Maoni