WALIKUWA WANAFUNZI KABLA YA KUWA MITUME WA YESU


 "Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume" Luka 6:13.

Hiyo inamaanisha kuwa kabla ya kujihusisha na utumishi lazima uwe mwanafunzi wa Yesu, Yesu aliwaita mitume kutoka miongoni mwa wanafunzi wake.

Uanafunzi ndio unazaa utumishi, usitake au usijihusishe na utumishi kabla ya kuwa mwanafunzi.

Narudia tena kwa herufi kubwa "UANAFUNZI NDIO UNAZAA UTUMISHI" LAZIMA UFUNDISHWE AU UJIFUNZE.

Hiyo ni kanuni ya falme zote (ufalme wa Mungu na ufalme wa giza).

👉Sauli alilelewa na Gamalieli akafundishwa hatimaye akawa Farisayo aliyekuwa mpinga Kristo wa zama hizo (Matendo ya Mitume 22:3-5).

👉Wachawi unaowajua, uliosoma habari zao kwenye Biblia au unaowasikia, KUNA MAHALI WALIFUNDISHWA HUO UCHAWI.

👉Waganga wa kienyeji unaowajua, uliosoma habari zao kwenye Biblia au unaowasikia, KUNA MAHALI WALIFUNDISHWA HUO UGANGA (Matendo ya Mitume 19:19).

NAHITIMISHA

1. Kabla ya kujihusisha na kazi ya kumtumikia Mungu, hakikisha unakuwa mwanafunzi wa Yesu, kumbuka kuwa kabla Yesu hajawaita mitume walikuwa wanafunzi wake (Luka 6:13).

2. Mungu anataka watumishi wanafunzi (disciple servants).

3. Kuwa mwanafunzi wa Yesu kwa kuweka neno la Mungu kwa wingi moyoni mwako (Yohana 8:31).

4. Kuwa mwanafunzi wa Yesu kwa kujifunza kutoka kwa wanafunzi wa Yesu (Mathayo 28:19-20) wanafunzi wa Yesu wanayo mafundisho waliyofundishwa na Yesu, unaweza kujifunza kwa wanafunzi wa Yesu kupitia kusoma Biblia au vitabu walivyoandika watumishi wa Mungu au kuhudhuria mafunzo kwenye vyuo au shule za huduma au utumishi ambazo zimeanzishwa na watumishi wa Mungu.

Chapisha Maoni

0 Maoni