HAKIKISHA WANAKULA - LISHA KONDOO ZANGU


 Hili ni maalumu kwa ajili ya wahubiri au wakufunzi wa neno la Mungu.

Kuhubiri na kufundisha ni kuwalisha watu vitu vya kiroho, ndio maana Yesu alimwambia Mtume Petro "lisha kondoo zangu". YOHANA 21:17.

 Jukumu lako kama mhubiri au mkufunzi wa neno la Mungu ni KUHAKIKISHA WATU WANAKULA - LISHA KONDOO 

DONDOO CHACHE KUHUSU KULA

1. Watu wanapokula huwa wanafungua midomo hakuna anayekula akiwa amefunga mdomo, watu wanapokula utawasikia wakitafuna au vijiko vikigonga sahani au wakisifia chakula au wakisema ongeza chumvi kidogo au ongeza sukari kidogo nakadhalika, vivyo hivyo wewe kama mhubiri au mkufunzi wa neno la Mungu UNAPASWA KUWAANGALIA WATU ILI UONE KAMA WANAKULA UNACHOWAPA AU HAWALI ILI IKUSAIDIE KUWAONA WASIOKULA NA UWASAIDIE KULA UNACHOWAPA.

Pia wakati unahubiri au kufundisha ni muhimu ujizoeze kumsikiliza Roho Mtakatifu ambaye anawajua vizuri hao watu ambao umesimama mbele zao, Roho Mtakatifu atakupa maneno ya kusema, mifano ya kutumia, atakuongoza kuwasimilia shuhuda ambazo zitawafanya wale unachowapa.

👉Kama wanakula utaona ishara mbalimbali kama vile kukuangalia kwa makini, kusikiliza kwa makini, kuandika nakadhalika. 

2. Kila mtu ana ulaji wake, kuna wanaokula haraka haraka, kula wanaokula taratibu, kuna wanaowahi kushiba, kuna wanaochelewa kushiba, vivyo hivyo unapowalisha watu vya rohoni kuna ambao wanaowahi kushiba (wanaokula haraka ndio wale wanaoelewa kwa haraka, wanaokula taratibu ndio wale wanaochelewa kuelewa) wale wanaochelewa unaweza kuwasaidia kuelewa kwa kufafanusha mambo unayowapa au kwa kutumia mifano (ZABURI 119:30, MATHAYO 13:34, JUKUMU LAKO KAMA MHUBIRI AU MKUFUNZI NI KUWASAIDIA WOTE WALE UNACHOWAPA.

Chapisha Maoni

0 Maoni