WIVU sio hali ya kawaida japo katika ulimwengu wa mwili, wivu unaweza kudhaniwa kuwa ni hisia fulani LAKINI BIBLIA INATUAMBIA WIVU NI KITU CHA KIROHO, NI ROHO.
Roho ya wivu inaweza kusababisha madhara makubwa sana katika familia, fuatilia mifano hii michache.
MFANO WA KWANZA: KAINI NA HABILI (Mwanzo 4:1-8)
Sadaka ya Habili ilikubaliwa na Mungu lakini sadaka ya Kaini ilikataliwa.
Wivu ulimtesa sana Kaini, akaamua kumuua nduguye.
MFANO WA PILI: FAMILIA YA YAKOBO (Mwanzo 30:1-24)
Roho mojawapo iliyosumbua familia ya Yakobo ni roho ya wivu, wake za Yakobo ambao walikuwa ndugu walioneana wivu mpaka ikafika hatua wakawa tayari kuona Yakobo akilala na wasaidizi wa kazi za nyumbani (house girls).
Wivu huo ulipelekea Yakobo kuzaa na wasaidizi wa kazi za nyumbani.
BAADHI YA MADHARA YA ROHO YA WIVU KWENYE FAMILIA
1. Inaweza kusababisha mauaji, ndugu kuuana kama Kaini alivyomuua Habili.
2. Inaweza kusababisha kuinuka kwa mashindano, watu watakuwa wakishindana tu, yaani mtu yuko tayari kuona nduguye anakuwa chini tu siku zote.
Hakuna kusaidiana, mtu anakuwa na mtazamo kwamba nikimsaidia ndugu yangu atakuwa na maisha mazuri kunizidi, ni heri abaki hivyohivyo.

0 Maoni