KWA NINI UOMBE


 Ziko sababu nyingi sana kwa nini unapaswa kuomba bila kukoma, zifuatazo ni baadhi ya sababu kwa nini unapaswa kuomba.

1. Kwa sababu maombi yanaweza kuzuia kuzuka, kuongezeka na kuimarika kwa maadui zako, zingatia haya mambo matatu

a). Kuzuka kwa maadui (1 Wafalme 11:14,23)

Kuzuka kwa adui ni pale ambapo maadui wanatokea ghafla, haujatarajia kama mtu au watu fulani watakuwa maadui zako au haujatarajia katika mazingira fulani utakutana na maadui. 

b. Maadui kuongezeka (idadi ya maadui kuongezeka) Zaburi 25:19

c. Kuimarika kwa maadui zako (pale ambapo maadui zako wana nguvu kukushinda wewe) 2 Samweli 22:18 

2. Kwa sababu hujui nani atakuwa adui yako baada ya muda fulani.

Mzazi au wazazi wanaweza kuwa maadui zako, ndugu zako wanaweza kuwa maadui zako, rafiki zako wanaweza kuwa maadui zako, mtoto au watoto wako wanaweza kuwa maadui zako, uliowaajiri wanaweza kuwa maadui zako, aliyekuajiri anaweza kuwa adui yako, mchungaji wako au askofu anaweza kuwa adui yako nakadhalika.

Habili hakujua kama kaka yake (Kaini) anawaza kumuua.

OMBA 

Chapisha Maoni

0 Maoni