NAO UNA VIUNGO VINGI


 Wakristo kutojua nafasi zao na wakristo kutokukaa kwenye nafasi zao kunasababisha matatizo mbalimbali kwenye mwili wa Kristo (kanisa).

(1 Wakorintho 12:12,14-25)

Mwili wa Kristo (kanisa) limefananishwa na mwili wa mwanadamu wenye viungo vingi, vinavyoonekana dhahiri na visivyoonekana dhahiri.

Mkono ukikaa mahali pa mguu, kutakuwa na shida, mguu wa kulia ukikaa mahali pa mguu wa kushoto lazima kutakuwa na shida kwenye mwili na muonekano, pua likikaa mahali pa jino lazima kutakuwa na shida kubwa kwenye mwili, jicho likikaa mahali pa kidole lazima kutakuwa na shida kubwa kwenye mwili na muonekano utakuwa sio mzuri.

Mitume wabaki kwenye utume, manabii wafanye walichoitiwa, waalimu wafanye walichoitiwa, wachungaji wafanye walichoitiwa, wainjilisti wafanye walichoitiwa, wenye kukirimu wafanye walichoitiwa nakadhalika.

Kila mmoja akitambua nafasi yake (wajibu wake na mipaka yake) hakutakuwa na shida kwenye mwili wa Kristo.

Chapisha Maoni

0 Maoni