👉Anza kumtumikia Mungu tu, acha kutazama madhaifu yako na dosari zako, ATUTENGENEZAYE NI MUNGU, USIJIPE KAZI YA KUJITENGENEZA, ACHA MUNGU AKUTENGENEZE.
Isaya 6:5-8
NDIPO NILIPOSEMA, OLE WANGU! KWA MAANA NIMEPOTEA; KWA SABABU MIMI NI MTU MWENYE MIDOMO MICHAFU, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi.
6. Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu;
7. AKANIGUSA KINYWA CHANGU KWA KAA HILO, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa.
8. Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.
(Ukitaka kuelewa vizuri habari hiyo hapo juu kuhusu Nabii Isaya anza kusoma mstari wa kwanza katika sura hiyo, nimekuandikia hayo machache kwa ajili ya kuhusihanisha na mada ninayofundisha ili uelewe kwa haraka).
Sio Nabii Isaya tu aliyekuwa na dosari za kimaadili na kiroho, hata mitume wa Yesu nao walikuwa na dosari za kimaadili na kiroho lakini Bwana Yesu aliwatengeneza, unafikiri Yesu alikuwa hajui Yuda alikuwa mwizi na anapenda sana fedha, Yesu alikuwa anajua hayo lakini Yuda alikuwa ni mmoja wa wale mitume kumi na wawili (Yohana 12:4-6).
👉Tatizo sio madhaifu au dosari zako za kimaadili na kiroho, TATIZO NI PALE UNAPOKATAA KUTENGENEZWA NA MUNGU.

0 Maoni