FAHAMU HAYA KUHUSU AYUBU


 AYUBU hakuwahi kushika maiki na kuhubiri injili, hakuwahi kutoa sadaka ili kupeleka injili, hakuwahi kuimba kwaya, hakuwahi kupiga chombo chochote cha muziki kwa ajili ya Mungu, hakuwahi kufanya uinjilisti wa nyumba kwa nyumba nakadhalika ILA MUNGU ALISEMA AYUBU NI MTUMISHI WAKE (Ayubu 42:7-8).


AYUBU ALIMTUMIKIAJE MUNGU?

(Ayubu 29:12-25)

1. Alisaidia masikini, yatima na wajane.

2. Alikuwa macho kwa vipofu (aliwaonesha njia vipofu) pia alikuwa miguu kwa viwete.

3. Alitetea haki za watu (haki za binadamu).

4. Alishughulika na watu walioonea na kutesa wengine.

5. Alikuwa mshauri wa watu.

6. Aliwaonesha watu njia wanayopaswa kuiendea.

7. Alifariji wengine na kuwapa matumaini waliokata tamaa.

👉ACHA UVIVU, kazi za kufanya ni nyingi kwenye ufalme wa Mungu, Anza kumtumikia Mungu sasa.

Chapisha Maoni

0 Maoni