Kukata tamaa ni tatizo linalowapata watu wengi sana, watu hujikuta wamekata tamaa kutokana na sababu mbalimbali kama vile majibu ya maombi yanapochelewa (soma Zaburi 69:3)(Zaburi 6:6).
Watu hukata tamaa kutokana na ugumu wa maisha (Soma 2 Wafalme 7:3-4)
Watu hukata tamaa kutokana na changamoto za ndoa au mahusiano, magonjwa na majaribu mbalimbali.
Watu hukata tamaa kutokana na misukosuko mbalimbali ya kihuduma au kiutumishi (1 Wafalme 19:2-5)
BAADHI YA AINA ZA KUKATA TAMAA
1.Kukata tamaa ya kuishi (2 Wakorintho 1:8)
Kukata tamaa ya kuomba (Luka 18:1)
2.Kukata tamaa ya kumtumikia Mungu (Yeremia 20:7-9)(Hesabu 11:11-15)
3.Kukata tamaa ya kuendelea mbele (Hesabu 14:1-4)
Kukata tamaa hupelekea watu kufanya mambo mbalimbali kama vile;-
1.Kumdharau, kumnung'unikia Mungu na kumkufuru Mungu (Ayubu 2:7-9)
2.Kujiua
3.Kufanya maamuzi yanayohatarisha maisha yao
4.Kukata tamaa huweza kusababisha watu kutengana (1 Wafalme 19:3) Nabii Eliya alipokata tamaa alitengana na mtumishi wake kule Bersheba.
5.Kukata tamaa hupelekea watu kuomba vibaya (1 Wafalme 19:2-4) Nabii Eliya alipokutana na misukosuko katika utumishi wake ilifika hatua akaanza kumuomba Mungu amuue.
BAADHI YA HATUA ZA KUCHUKUA UNAPOKATA TAMAA
Tambua chanzo kilichopelekea ufikie hatua ya kukata tamaa.
(Luka 15: 11-18) Mwana mpotevu alijikuta yuko kwenye hali mbaya ya kimaisha, hali ya kuvunja moyo lakini alitambua chanzo kilichosababisha afike hapo alipofika ni uovu akaamua kutubu. Kutubu kukawa mwanzo wa mabadiliko ya maisha yake.
Kuna watu wamejikuta na magonjwa, mateso, dhiki kutokana na uovu wao, wako katika hali ya huzuni na majuto.
Ili utoke hapo kiri ulikosea na uombe msamaha kwa Mungu na kwa uliyrmkosea.
Mtwike Mungu fadhaa zako (1 Petro 5:7)
Fadhaa ni huzuni, masikitiko, huzuni au mambo yote yanayokufadhaisha.
Yesu alipokuwa na huzuni alimuomba Baba yake na akatiwa nguvu, akapata msaada (Mathayo 14:33-36).
Omba Mungu akutie nguvu (Mithali 24:10)
Biblia inasema kukata tamaa hudhihirisha kwamba nguvu zako ni chache ili uondokane na hali hiyo unapaswa kupata nguvu.
Omba Mungu akutie nguvu.

0 Maoni