UHUSIANO WA NAFASI YAKO NA THAMANI YAKO


Wakati mwingine watu hawawezi kuona na kutambua thamani yako KWA SABABU HAUJAKAA KWENYE NAFASI YAKO AMBAYO MUNGU ANATAKA UKAE.

Yusufu aliwasimulia ndugu zake ndoto anazoota lakini ndugu zake walizidi kumchukia, wakapanga kumuua, wakabadilisha mpango wa kumuua hatimaye wakamuuza (Mwanzo 37:18-28), HAWAKUONA THAMANI YAKE.

Lakini ilipofika hatua Yusufu alipokaa kwenye nafasi yake ndipo THAMANI YAKE ILIANZA KUONEKANA.

KWA NINI NIMEKUTAZAMISHA JAMBO HILO?

Ni kwa sababu nataka ufahamu kuwa wakati mwingine watu hawatona thamani yako kama haujakaa kwenye nafasi yako.

Wakati mwingine jizoeze kumuomba Mungu AKUWEKE KWENYE NAFASI AMBAYO UNAPASWA KUWA (Zaburi 118:5).



Chapisha Maoni

0 Maoni