USIDHARAU


 Wakati mwingine Mungu huwa anaamua kumwambia mtu fulani mambo ya msingi sana hata kama mtu huyo hamuabudu Mungu huyo.

Kwa mfano

1. Alimfunulia Mfalme Farao kuhusu miaka Saba ya shibe na miaka Saba ya njaa inayokuja (soma kitabu cha Mwanzo sura ya 31).

2. Alimfunulia Mfalme Nebukadneza mambo mazito sana yahusuyo nyakati za mwisho na mustakabali wa dunia (Soma kitabu cha Danieli sura ya 2).

👉Usidharau ndoto za watu wanazoota kuhusu wewe hata kama watu hao hawajawahi kuwaza kwenda kanisani kusali. 

👉Usidharau ndoto za watu wanazoota kuhusu wewe hata kama sio waadilifu.

👉Usidharau ndoto za watu wanazoota kuhusu nchi au eneo fulani hata kama watu hao hawamuabudu Mungu. 

✍️MUNGU ANAFANYA KAZI ZAKE ZAIDI YA SISI WANADAMU TUNAVYOFIKIRI.

Chapisha Maoni

0 Maoni