SHERIA ZA UTUMISHI KATIKA UFALME WA MUNGU


 Kila ufalme au serikali huweka sheria za utumishi ambazo zinapaswa kufuatwa au kuzingatiwa na kila mtumishi katika ufalme au serikali hiyo.

Vivyo hivyo katika ufalme wa Mungu kuna sheria mbalimbali za utumishi katika ufalme huo ambazo zinapaswa kufuatwa au kuzingatiwa na kila mtumishi.

SHERIA MOJAWAPO YA UTUMISHI KATIKA UFALME WA MUNGU

Ni kuyatenda mapenzi ya Mungu.

Mungu anataka mapenzi yake yatimizwe hapa duniani kama yanavyotimizwa kule mbinguni (Mathayo 6:10). Mungu hataki umtumikie tu, Mungu anataka uyatende mapenzi yake wakati unamtumikia.

Bwana Yesu alisema waziwazi kwamba "KUNA WATUMISHI ATAWAKATAA KWA SABABU WALIKUWA HAWATENDI MAPENZI YA MUNGU" japo watamuambia walifanya miujiza, walitoa pepo kwa jina lake, walitoa unabii kwa jina lake nakadhalika lakini atawaambia SIKUWAJUA KAMWE (Mathayo 7:21-23).

Yesu mwenyewe alipokuwa duniani ALIZINGATIA SANA SHERIA HII YA KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU (Mathayo 12:50)(Mathayo 26:42)(Yohana 4:34)(Yohana 5:30).

ZINGATIA sana sheria hiyo☝️☝️☝️

Chapisha Maoni

0 Maoni