KUHUSU MUNGU KUJIBU MAOMBI YAKO - SEHEMU YA PILI


 Kuna wakati Mungu hajibu maombi sio kwa sababu umeomba vibaya au kwa sababu una dhambi ILA NI KWA SABABU IMANI YAKO IMEKOSA MATENDO (Yakobo 2:27-18).

Kwa mfano unaomba Mungu akufanikishe kupata kazi lakini hautumi barua za maombi ya kazi, hautafuti kazi, umekaa ndani na vyeti tu, hauko tayari kutafuta kazi, NI KWELI UNA IMANI MUNGU ANAWEZA KUKUFANIKISHA LAKINI HAUNA MATENDO, sio rahisi kupokea majibu ya maombi yako kutoka kwa Mungu (Mathayo 7:7).

Kwa mfano unamwomba Mungu unataka akufanikishe kuwa Rais, mbunge, diwani nakadhalika lakini hauchukui hatua ya kujiunga na vyama vya siasa na kugombea nafasi hizo, sio rahisi Mungu kujibu maombi hayo.

Kwa mfano unaomba Mungu akutumie kwa viwango vikubwa kama Askofu Idahosa, Mzee TL Osborn, Mtume Paulo, Reinhard Bonke, Mzee Mwakasege, Mzee Kulola nakadhalika lakini ukiambiwa kufunga masaa kumi na mbili tu unaanza kusingizia una madonda ya tumbo, una minyoo nakadhalika, UNAAMINI KABISA MUNGU ANAWEZA KUKUTUMIA ILA HAUKO TAYARI KULIPA GHARAMA FULANI WALIZOLIPA WATUMISHI HAO, MUNGU HAWEZI KUKUTUMIA KWA VIWANGO HIVYO.

Niishie hapa kwa sasa natumaini umenielewa.

Chapisha Maoni

0 Maoni