Wakati mwingine Mungu hajibu maombi sio kwa sababu umeomba vibaya au kwa sababu una dhambi ILA NI KWA SABABU UNAOMBA MAMBO AMBAYO YAKO NDANI YA UWEZO WAKO.
Watu wengi hawafahamu kuwa ndani yetu Mungu aliweka uwezo wa ajabu sana ila mara nyingi shetani huwa anahakikisha anakukandamiza ili usiuone uwezo uliopewa, kila ukijitazama unajiona mnyonge, dhaifu, hauna pa kuanzia nakadhalika.
Wakati mwingine muombe Mungu afungue macho yako ili uone uwezo alioweka ndani yako, ukiuona uwezo ambao Mungu ameweka ndani yako KUNA MAMBO UTAACHA KUMUOMBA MUNGU.
Ukipata nafasi soma
Waamuzi 6:14. Bwana akamtazama (Gideoni), akasema, Enenda KWA UWEZO WAKO HUU ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?
---------------
Then the Lord turned to him and said, "Go in this MIGHT OF YOURS, and you shall save Israel from the hand of the Midianites. Have I not sent you?"

0 Maoni