KUTUNZA ARDHI


 Kati ya jambo ambalo tumefanya wanadamu na linatugharimu ni uharibifu wa ardhi ambayo Mungu alitupatia.

Tangu mwanzo Mungu alimwambia Adamu ailime ardhi na kuitunza (Mwanzo 2:15), kuitunza ardhi lilikuwa ni jambo lenye manufaa kwake mwenyewe, kwa uzao wake na kwa dunia kwa ujumla.

Mungu mwenyewe amekuwa mfano bora wa utunzaji wa ardhi tangu mwanzo (Mwanzo 2:5-6), Biblia inasema "wewe waitunza nchi (ardhi) kwa kuinyeshea mvua, waijalia rutuba na kuistawisha; mto wako umejaa maji tele, waifanikisha nchi na kuipatia mavuno. Hivi ndivyo uitengenezavyo nchi (Zaburi 65:9).

BAADHI YA MBINU ZA KUTUNZA ARDHI

1. Kutunza vyanzo vya maji.

2. Kupanda miti na kurejesha miti. 

3. Kuondoa takataka kwenye uso wa ardhi, Mungu ameweka mifumo ya ukusanyaji na uondoaji taka kwenye ardhi, kwa mfano kuna ndege na wanyama ambao wanakula mizoga, kuna viumbe wengine ambao wanakula takataka, kwa mfano funza nakadhalika. Mungu aliwaumba kwa ajili ya kusudi lake ikiwemo kutunza mazingira. 

Sisi kama wanadamu lazima tuwe na mifumo inayotusaidia kutunza ardhi kwa manufaa yetu wenyewe.

4. Epuka kumwaga damu kwa njia yoyote, umwagaji damu huinajisi ardhi.

5. Kuiacha ardhi ipumzike, ardhi ni kiumbe kama viumbe wengine vinahitaji kupumzika ili vifanye kazi kwa ufanisi ili kumnufaisha mwanadamu ndio maana Mungu aliwaagiza waisraeli waipumzishe ardhi kwa mwaka mmoja (Kumbukumbu la torati 23:10-11).

6. Umwagiliaji, umwagiliaji ninaouzungumzia sio ule unaofanyika kwenye kilimo, namaanisha kumwagilia maji ardhi hata kama hakuna kilimo kinafanyika, Mungu sio mkulima wa zao lolote la chakula au la biashara ila huwa anaimwagilia maji ardhi kwa manufaa ya wanadamu (Zaburi 65:9).

BAADHI YA MADHARA YA KUHARIBU ARDHI 

1. Ukosefu wa usalama wa chakula.

2. Uwepo wa maradhi.

3. Uwepo wa hewa chafu.

4. Ardhi kukosa rutuba.



Chapisha Maoni

0 Maoni