JINSI TUNAVYOPASWA KUWATAZAMA WASIOAMINI


 UTANGULIZI

Kumekuwepo na shida ya kiufahamu miongoni mwa baadhi ya wahubiri wa injili za mitaani, shida yenyewe ni kutowatazama wasioamini kama jinsi Mungu anavyowatazama.

Kutokana na shida hiyo ya ufahamu ndio maana unaweza kusikia kauli kama hizi "wachawi wananuka midomo" au "wachawi hawana akili" au "usipotubu utakufa" au "kuwatishia watu ili waokoke waepuke Jehanamu" nakadhalika.

Hapa nataka niweke msisitizo kidogo kama ifuatavyo;-

1. Wewe mhubiri usijifanye una uchungu sana kuliko Yesu aliyewafia watu msalabani, Yesu ndiye mwenye uchungu na wanadamu kwa kuwa alilipa gharama kubwa kuwakomboa ILA ANAWATAZAMA KWA JICHO LA UPENDO WA AJABU SANA, acha hasira zako nyumbani, usiende kuhubiri injili ukiwa na ghadhabu.

Yesu hakuja kuhukumu ulimwengu bali kuokoa (Yohana 12:47)(Yohana 8:11) (Luka 19:10)

2. Injili sio vitisho, kejeli, sio kitega uchumi, sio fursa ya kuonyesha umwamba nakadhalika, INJILI NI HABARI NJEMA, NI UWEZA WA MUNGU ULETAO WOKOVU (Warumi 1:16)(Warumi 10:15).

Imekuwa si ajabu kusikia mhubiri akisema "wachawi hamniwezi" au "kama mnaweza njooni mjaribu muone" 

Mambo kama hayo ni madhihirisho ya kwamba HUYU MHUBIRI HAJUI ANACHOKIFANYA, HATAZAMI WASIOAMINI KAMA MUNGU ANAVYOWATAZAMA.

JINSI TUNAVYOPASWA KUWATAZAMA WASIOAMINI

1. WASIOAMINI NI WAGONJWA WANAOHITAJI TABIBU

(Mathayo 9:12)

Yesu aliwaita wenye dhambi au wasioamini ni wagonjwa wanaohitaji tabibu. Hakuna daktari anayemtishia mgonjwa au kumfanya mgonjwa akate tamaa hata kama yuko katika hali mbaya.

Mhubiri wa injili ni kama daktari anayehudumia wagonjwa, lazima mhubiri uwe na lugha ya upendo, lazima uwe na maneno safi (habari Njema) ambayo mtu akiisimia anatiwa moyo na anafungiwa utayari wa kuamini injili.

Injili ni dawa hasa, hubiri injili ACHA KELELE NA UJINGA.

2. WASIOAMINI NI WATOTO WA MUNGU WALIOPOTOEA

Isivyo bahati (bahati mbaya) watu wengi au wahubiri wengi husahau kuwa Yesu alifundisha kuhusu kisa kinachojulikana kama "KISA CHA MWANA MPOTEVU" (Luka 15:10-32).

Kisa hicho kinatupa ufahamu kuwa Mungu anawatazama wenye dhambi au wasioamini kama WATOTO WAKE WALIOPOTOEA.

Kwa hiyo nao wanapaswa kuupata uzima wa milelel kwa kuwa nao ni watoto wa Mungu ILA WAMEPOTEA TU 

Kazi ya injili ni kuwarudisha nyumbani watoto wote wa Mungu ili wapate Zawadi yao ambayo ni uzima wa milele.

Kwa hiyo unapokwenda kuhubiri injili USIDHANI UMEKWENDA KWA WATU AMBAO NI TAKATAKA AU WATU AMBAO MUNGU ANAWACHUKIA.

Fahamu kuwa wasioamini ni watoto wa Mungu waliopotea, Mungu anawataka ili wapate uzima wa milele.

HITIMISHO

Ili uwe mhubiri mzuri wa injili, jambo mojawapo unalopaswa kujifunza ni namna ya kuwatazama wasioamini au jinsi Mungu anavyowatazama wasioamini, ukifahamu jinsi Mungu anavyowatazama wasioamini HUWEZI KUWAKEJELI AU KUWAHUBIRI HUKU UMEJAA GHADHABU NAKADHALIKA.

Utawahubiri kwa nguvu ya upendo wa Mungu juu yao na injili itazaa matunda. 

Chapisha Maoni

0 Maoni