VIJENGAVYO NA VIBOMOAVYO


 ✓Kama kuna vinavyojenga basi kuna vinavyobomoa.

✓Kama kuna vinavyobomoa basi kuna vinavyobomoka.

✓Kama kuna vinavyobomoka basi epuka vinavyobomoa.

✓ "Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo" 1 Wakorintho 10:23. 

✓ Kama kuna vinavyojenga basi kuna vinavyojengwa.

KWA MFANO

1. Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe ila mpumbavu hubomoa, kama unataka kujenga lazima ujue vitu gani vinajenga na vitu gani vinabomoa (Mithali 14:1).

2. Nafsi inajengwa, ukitaka kujenga nafsi yako lazima ujue mbinu mbalimbali za kujenga nafsi (1 Wakorintho 14:4).

3. Kanisa linajengwa na vitu mbalimbali (1 Wakorintho 14:5)(2 Wakorintho 13:10), ili kanisa lijengwe lazima zitumike zana au nyenzo za kujengea.

5. Mtu anajengwa (1 Wathesalonike 5:11), kuna mambo yanayoweza kumjenga mtu.

6. Mwili unajengwa, lazima ufahamu vitu vinavyoweza kuujenga mwili (

FAHAMU HAYA MACHACHE KAMA UNATAKA KUJENGA

1. Lazima ukubali kulipa gharama, huwezi kujenga chochote bila kulipa gharama (Luka 14:28-30).

2. Huwezi kujenga chochote bila nguvu (ujuzi, maarifa, fedha, hekima, upendo nakadhalika).

3. Huwezi kujenga bila kuweka msingi, kama unataka kujenga chochote lazima ujue jinsi ya kuweka misingi (1 Wakorintho 3:10) na aina za misingi kutegemeana na unachotaka kujenga. Hata Mungu akitaka kujenga huwa anaweka msingi kwanza, kwa mfano kabla Mungu hajaumba ulimwengu aliweka msingi kwanza (Luka 11:50)(Waebrania 9:26)(Zaburi 102:25)(Zaburi 89:11).


Chapisha Maoni

0 Maoni