UTANGULIZI
Kila mmoja wetu amewahi kusafiri kwa kutumia vyombo mbalimbali kama vile boti, meli, treni, ndege nakadhalika.
Kila mtu anaposafiri huwa kuna mahali anaelekea (kituo) haijalishi anasafiri kwa kutumia aina Fulani ya usafiri ila kila mtu huwa kuna mahali anakwenda. Kila mtu anapofika mahali anapokwenda (kituo chake) huwa anashuka na hapo ndipo unakuwa mwisho wa safari yake.
MAISHA NI KAMA SAFARI
1 Petro 2:11. Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
Sisi wote ni wasafiri na wapitaji hapa duniani, kwa kuwa kila msafiri huwa ana kituo chake ambacho akifika hapo anakuwa amefika anakokwenda, kifo ni kituo cha viumbe hai ikiwemo mwanadamu.
Kila mtu ana kituo chake cha kushukia, siku ya kufa au saa ya kufa ndio kituo chako cha safari yako ya hapa duniani.
Ukishuka kwenye hicho kituo kuna njia mbili tu ambazo ni (1) njia ya kwenda uzimani (2) njia ya kwenda mautini.
Njia ya kwenda uzimani ni njia ya kukupeleka moja kwa moja kwa Mungu ila njia ya kwenda mautini ni njia ya kwenda Jehanamu ambapo atatupwa shetani na malaika zake.
Yesu Kristo ndiye njia ya kwenda uzimani (Yohana 14:6), ukifa nje ya Yesu Kristo au ukifa huku haujamwamini Yesu utakuwa umechagua kwenda kwenye njia iendayo mautini.
HITIMISHO
Kwa kuwa sisi wote ni wasafiri na wapitaji hapa duniani na kituo chetu wote ni kifo, lazima ujiandae ili ikifika siku ya kushuka kwenye kituo chako (siku ya kufa) uwe na uhakika wa usalama wako.
Ili uone raha na amani ukishuka kwenye kituo chako ni heri umwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na afanyike mwokozi wa maisha yako (Warumi 10:9-10).

0 Maoni