KINYESI CHA NDEGE JUU YA KICHWA CHAKO


Ndege hupita juu yetu (angani - hewani) wakati mwingine kinyesi chao hutuangukia kichwani au begani au kwenye nguo LAKINI HAKUNA AMBAYE UHANGAIKA KUMTAFUTA NDEGE HUYO ILI AMUADHIBU, HAKUNA AMBAYE HUPANGA MPANGO WA KISASI KWA AJILI YA NDEGE HUYO, huwa tunaondoa kinyesi, tunajisafisha na tunaedelea na mambo mengine.

Nachotaka kukufundisha ni kwamba JIFUNZE NA JIZOEZE KUPUUZIA MAMBO MBALIMBALI kama vile masimango, dharau, dhihaka nakadhalika. Ukijifunza na kujizoeza kupuuzia mambo mbalimbali itakusaidia;-

1. Kutopoteza nguvu zako.

2. Kutopoteza muda wako ovyo.

3. Kuepuka msongo wa mawazo, uchungu kwenye moyo, hasira nakadhalika.

4. Kulinda moyo wako.

5. Kutunza heshima yako. 

NB: Mambo mengine yachukulie kama mavi ya ndege yaliyokuangukia, ACHA KUHANGAIKA KUMPATA NDEGE ALIYEKUNYEA ILI UMUADHIBU, UTAJICHOSHA, UTAPOTEZA MUDA, NGUVU NAKADHALIKA.

Chapisha Maoni

0 Maoni