✓Kanisa lilimlilia Mungu kupitia maombi kwa ajili ya Mtume Petro aliyekuwa amewekwa gerezani ili baada ya Pasaka auawe, kanisa lilipomwomba Mungu alimuepusha Mtume Petro na kifo (Matendo ya Mitume 12:1-12)
HITIMISHO
Ni heri kumlilia Mungu akuepushe na mambo mbalimbali, ukiacha kumlilia Mungu unaweza kujipata una kilio ambacho kingeweza kuepukika endapo ungemwomba Mungu.
Kwa kumlilia Mungu kupitia maombi unaweza ukaepuka vilio vingi ambavyo vinaweza kuepuka endapo utamuomba Mungu, lia kabla haujalia.
Omba sasa kwa ajili yako mwenyewe, kwa ajili ya familia yako, kwa ajili nchi yako nakadhalika, LIA KABLA HAUJALIA.

0 Maoni