MBINU NYINGINE YA KIBIBLIA YA KUKUSAIDIA KUZAA MTOTO AU WATOTO


 Fundisho hili ni mahsusi kwa ajili ya wanawake ambao wamekuwa wakitamani kuzaa watoto na hawajapata watoto (wagumba, tasa, waliotolewa vizazi au waliofungwa matumbo yao ya uzazi).

UTANGULIZI

Ukisoma Biblia utagundua kuwa kuna aina mbili za upatikanaji wa watoto, aina ya kwanza ni ile ya kupata watoto kwa njia ya kawaida yaani kuzaa bila agano lolote na Mungu.

Aina ya pili ya upatikanaji wa watoto ni ile ya kuweka nadhiri za kupata watoto.

BAADHI YA WATU WALIOTUMIA MBINU YA KUWEKA NADHIRI NA WAKAPATA WATOTO

1. Mama yake na Mfalme Lemueli (Mitahli 31:1-2)

Biblia haituambii kwa uwazi sana kuhusu nadhiri aliyoweka mama yake Lemueli ila Biblia inatujulisha kuwa Mfalme Lemueli ni mtoto aliyezaliwa kutokana na nadhiri ambazo mama yake aliweka kwa Mungu, rejea (Mithali 31:1-2).

2. Mama yake Nabii Samweli (1 Samweli 1:9-10, 19-20)

Hana alikuwa mke wa mtu mmoja aliyeitwa Elikana, Elikana alikuwa na wake wawili ambao ni Penina na Hana, Penina alikuwa na watoto lakini Hana hakuwa na watoto, Penina alimsimanga sana Hana mpaka akawa anakosa raha.

Sikumoja Hana alikwenda mbele za Mungu alimlilia Mungu sana na akaweka nadhiri kwamba Mungu akimpa mtoto wa kiume atamtoa huyo mtoto akamtumikie Mungu sikuzote za maisha yake, baada ya nadhiri hiyo Mungu alimkumbuka Hana na akafungua tumbo lake hatimaye Hana alipata mtoto ambaye ni Nabii Samweli.

3. Mama yangu mimi Faraja Gasto

Moja ya simulizi ambayo mama yangu mimi amekuwa akiisimulia ni namna ambavyo alisumbuka sana kwa kutokuzaa, anasema sikumoja alimlilia Mungu akaweka nadhiri akasema "Mungu ukinipa mtoto wa kike au wa kiume" nitamtoa kwako akutumikie sikuzote.

Mungu alimsikia hatimaye mimi nilizaliwa.

HITIMISHO

Kuweka nadhiri ni mbinu ambayo imewasaidia watu wengi kupata watoto, kama umekuwa unasumbuka na matatizo ya uzazi unaweza ukatumia mbinu hii ambayo imewahi kuwanufaisha watu wengi sana.

Angalizo: baada ya kupata mtoto au watoto hakikisha unafanya sawasawa na nadhiri uliyoweka, usije kuthubutu kukosa uaminifu.

Chapisha Maoni

0 Maoni