Faraja Gasto
Kila
kiongozi (wa kidini, kisiasa n.k) anatakiwa kutunza au kulinda ushawishi wake
(influence) ili asiupoteze.
Kila
mtu anayetaka kupata nafasi fulani ya uongozi anatakiwa kutafuta kuwa na
ushawishi.
Ushawishi
ni moja ya nguzo muhimu sana inayosababisha watu wamchague mtu fulani kuwa
kiongozi, ushawishi husababisha watu wamuamini na wamtii kiongozi au wakubali
kuongozwa na mtu fulani.
Ushawishi
unaweza kuongezeka, kupungua, kupotea na kuimarika kutegemeana na mambo
mbalimbali kama vile tabia ya kiongozi, misimamo ya kiongozi n.k
Ili
uweze kupata, kulinda, kuongeza na kuimarisha ushawishi wako.
1.
Jenga tabia ya kuheshimu watu.
2.
Wajali watu
-Lia
na wanaolia pia cheka na wanaocheka.
-Wajulie
watu hali.
-Jitolee
kuwasaidia watu.
3.
Uwe mfano wa kuigwa katika mambo yote.
4.
Uwe na msimamo.
-Simamia
ulichosema bila kubadilikabadilika.
5.
Uwe mwaminifu.
-Timiza
ahadi zako.
-Heshimu
makubaliano.
6.
Jipatie maarifa toka kwenye vyanzo mbalimbali.
-
Kiongozi asiye na maarifa huwa anawahi kupoteza ushawishi.
0 Maoni