Lengo
la somo: ni kukufundisha namna ya kupanda fedha ili uvune
fedha.
Utangulizi
Kati ya vitu ambavyo
watu wanatamani kuwa navyo ni fedha. Tukitazama kwenye neno la Mungu tunaona Mungu
anasema fedha na dhahabu ni mali yake (Hagai 2:8).
Tena Biblia inasema
kwamba “fedha ni jawabu la mambo yote” (Mhubiri 10:19c)
Kwa sababu fedha ni
jawabu la mambo yote ndio maana kila mtu anafanya jitihada za kupata fedha japo
wapo wengine wanaotumia njia mbaya kupata fedha (wizi, kuuza miili, kuuza
vilevi n.k).
Biblia imetoa
tahadhari kwamba mtu yeyote hatakiwi kuipenda fedha maana shina moja la mabaya
yote ni kuipenda fedha (1 Timotheo 6:10).
ANGALIZO: Ijulikane
kuwa kutafuta fedha sio kupenda fedha ila kuipa fedha nafasi ya Mungu(nafasi ya
kwanza maishani mwako) huko ni kupenda fedha.
KOSA
AMBALO LINAWASABABISHIA WENGI WASIPATE FEDHA
Watu wengi wanaogopa kupanda fedha na wengine hawajui kuhusu
kupanda na kuvuna.
(Wagalatia 6:7)
“Msidanganyike Mungu
hadhihakiwi kwa kuwa chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna”
Chochote unachopanda
ndicho utakachovuna, kwa hiyo kama unataka fedha lazima ujifunze kupanda fedha
ili uvune fedha. Kama haupandi fedha usitarajie kuvuna fedha hata ukifunga na kuomba,
hakuna mahali popote kwenye Biblia panapoonyesha mtu alipata fedha bila
kuzipanda.
MBINU
ZA KUPANDA FEDHA
1.Jifunze
kuwekeza fedha (invest)
(Mathayo 25:14-27)
Huyu jamaa alipanga
kusafiri, kabla hajasafiri aliwekeza fedha zake kwa watumwa wake watatu,
watumwa wawili walilipokea zile fedha wakaziweka kwenye biashara ili ziweze
kuzaa faida, mtumwa mmoja hakuwekeza fedha aliyopewa.
Wale waliowekeza
walipata faida na ambaye hakuwekeza hakupata faida yoyote. Ninachotaka uone
hapo ni kwamba uwekezaji ni njia ya kupanda fedha, unapowekeza unakuwa umepanda
ipo siku utavuna.
Angalizo:
Yapo
makosa mengi ya kiuwekezaji ambayo yanawafanya watu wapate hasara mara baada ya
kuwekeza, kwa kuwa sifundishi kwa undani kuhusu uwekezaji napenda nikuonyeshe
kosa mojawapo linalowafanya watu wapate hasara mara baada ya kuwekeza. Kosa
lenyewe ni kutofahamu mahali sahihi pa kuwekeza kutegemeana na wakati husika,
mazingira unayowekeza na kiwango cha fedha. Ukisoma (Mathayo 25:14-27) utaona
huyo tajiri aliwekeza kwa watu anaowafahamu vizuri, watu anaofahamu uwezo wao.
Ingekuwa ni suala la biashara ningeweza kusema kwamba aliwekeza katika biashara
anayoifahamu vizuri.
Mahali sahihi pa
kuwekeza
1.Wekeza kwenye mambo
ya ufalme wa Mungu kama vile kutoa fedha kwa ajili ya kufanikisha mikutano ya
injili, kuwasafirisha watumishi wa Mungu, kusimama pamoja na watumishi wa
Mungu, kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa makanisa, ununuzi wa vyombo vya
injili n.k
2. Wekeza wenye
maisha ya watu, hili nitalizungumzia katika hiyo pointi namba mbili inayohusu
“kuwapa watu vitu”
2.Wape
watu fedha (give)
(Luka 6:38)
Biblia inasema
“wapeni watu vitu” ukiwapa watu vitu utapokea maradufu zaidi ya ulivyowapa.
Ukiwapa watu fedha utapokea fedha maradufu zaidi ya ulivyowapa.
Angalizo: Biblia
haisemi wape wakristo vitu, bali inasema wapeni watu vitu ila katika kuwapa
watu vitu hakikisha kipaumbele chako ni watu wa jamii ya waaminio (Wagalatia 6:10)
(Ayubu 29:1-17)
Ayubu anasema
alipokuwa ana hali nzuri ya kiuchumi alikuwa akiwapa watu vitu vyake. Kumbuka
huyu Ayubu alikuwa tajiri sana katika kipindi hicho na katika eneo alipokuwa,
siri mojawapo ya utajiri wake ni kuwapa watu vitu.
Panua
ufahamu wako kuhusu fedha
Ukitaja neno fedha watu wengi wataanza kuona
sarafu au noti kwenye ufahamu wao, fedha sio sarafu na noti tu, fedha ni pamoja
na kitu chochote chenye thamani.
Maana yake ni kwamba simu uliyonayo ni fedha, nguo
ulizonazo ni fedha, viatu ulivyoavyo ni fedha.
Nakumbuka mwalimu wangu aliyekuwa akinifundisha
somo liitwalo “Finance management” aliwahi kutufundisha kitu kinaitwa “cash
equivalent” yaani ni sawa na kusema kwamba
“kubadili ulichonacho kuwa fedha” (converting things into cash), Yule
mwalimu alitufundisha kwamba vitu ulivyonavyo unaweza kuvibadili vikawa fedha, kwa mfano kama una
saa ya mkononi hiyo ni fedha, kama una simu hiyo ni fedha. Njia mojawapo ya
kubadili hivyo vitu kuwa fedha ni kuuza hico kitu ndio maana Yesu aliwahi
kumwambia mtu Fulani “kauze ulivyonavyo kisha fedha wagawie maskini”.
Kwa hiyo suala la kuwapa watu vitu sio lazima uwe
na fedha mkononi, hata nguo, saa, mkoba n.k hizo ni fedha.
3.Wape watu taarifa za fursa au kazi
3.Wape watu taarifa za fursa au kazi
Mwl.Faraja Gasto
Mwanzilishi&Mwenyekiti wa Maarifa Team
+25567955334
farajagasto97@gmail.com/
farajagasto@yahoo.com
2 Maoni
Vyema kabisa,
JibuFutahakika huwezi kupanda usingizi ukavuna utajiri.
Tena
Huwezi panda uvivu ukavuna kufanikiwa.
Na pia...
Ukipanda malalamiko, ni lazima uvune malalamishi.
"Hakika! Apandacho mtu ndicho atakachovuna"
AHSANTE KWA MAKALA YAKO NZURI KABISA KWA USTAWI WA FIKRA ZETU.
Nakusalimu
Barikiwa
Futa