AGANO KAMA KUFURI NA UFUNGUO WA MALANGO MBALIMBALI


 UTANGULIZI

Jambo mojawapo lenye nguvu ni maagano, kupitia maagano watu wanaweza kufungwa au eneo linaweza kufungwa. Pia agano au maagano yanaweza kuwa funguo ya kufungua mbalimbali yaliyofungwa.

Kwa mfano kuna mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo nchi wanachama wamekubaliana nayo, mikataba hiyo ni agano au maagano ambayo nchi wanachama zimefungwa kwenye maagano hayo, nchi yoyote ikienda kinyume na agano hilo inaweza kuwekewa vikwazo nakadhalika kwa sababu kwenda kinyume na agano ni sawa na kuvunja kufuri kwenye mlango wa mtu mwingine.

AGANO KAMA FUNGUO YA KUWAFUNGULIA WAISRAELI MLANGO WA KUTOKA NCHINI MISRI

(Kutoka 2:23-25)

Wana wa Israeli walipatwa na mateso makali sana wakamlilia Mungu, "Mungu alikumbuka agano lake aliliofanya na Ibrahimu, Isaka na Yakobo" (Kutoka 2:24-25).

Lile agano ndilo lilikuwa funguo ya mlango w kutokea katika nchi ya Misri ambayo Mungu aliita ni nyumba ya utumwa kwa wana wa Israeli ( Kutoka 20:1).

HITIMISHO

Fahamu kuwa maagano yanaweza kuwa kufuri au funguo za malango mbalimbali, agano jipya ni funguo ya mlango wa mahusiano mapya na Mungu.

Je! uko tayari kurejesha mahusiano yako na Mungu? kama jibu ni ndiyo chukua ufunguo ambao ni agano jipya ufungue mlango wa mahusiano mapya na Mungu. Ili ujiunganishe kwenye agano jipya lazima umwamini Yesu Ili damu yake ya agano ikufungulie mlango wa mahusiano mapya na Mungu.


Chapisha Maoni

0 Maoni