KUPANGA (PLANNING)


 Mithali 16:9

✓Moyo wa mtu huifikiri NJIA YAKE; Bali Bwana huziongoza hatua zake. (Mithali 16:9 SUV).

✓Mtu aweza kufanya MIPANGO yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake (Mithali 16:9 BHN)

✓A man's heart PLANS his way, But the Lord directs his steps. (Proverbs 16:9 NKJV)

✓You may make your PLANS, but God directs your actions. (Proverbs 16: 9 GNB)

Nimekuwekea andiko la Mithali 16:9 kutoka kwenye aina kadhaa za Biblia ili kukurahisishia kuelewa nitakachofundisha kuhusu kupanga.

KUPANGA NI NINI?

Ni kukusudia kufanya jambo fulani, kwa lengo fulani, kwa muda fulani, kwa mbinu au njia fulani na kwa kutumia rasilimali au malighafi fulani. 

Kwa mfano Mungu alikusudia kuumba dunia na vilivyomo kwa muda wa siku sita, vingine viliumbwa kwa neno lake lakini mtu aliumbwa kwa udongo, neno na udongo vilikuwa malighafi au rasilimali ambazo Mungu alitumia kutimiza mpango wake wa uumbaji.

JE! TUNAPASWA KUPANGA MAMBO MBALIMBALI?

Ndio tunapaswa kupanga kwa kuwa neno la Mungu linasema "Mtu aweza kufanya MIPANGO yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake" (Mithali 16:9 BHN)

Lazima tupange tutaishi wapi, tutazaa watoto wangapi, tukiwa wazee tutaishije, watoto wetu wasome wapi, panga unataka kuwa na ndoa ya aina gani nakadhalika. 

Tukishapanga, Mungu anachofanya ni kuziongoza hatua zetu au kutusaidia namna bora ya kutimiza mipango hiyo.

AINA KADHAA ZA MIPANGO

1. Mipango ya mtu binafsi.

2. Mipango ya jumuiya, kikundi au timu fulani.

3. Mipango ya taasisi (familia, kampuni nakadhalika).

4. Mipango ya nchi. 

BAADHI YA MIPANGO AMBAYO MUNGU ANAIUNGA MKONO

1. Mipango ya watu kuokolewa (ushuhudiaji au uinjilisti) Marko 16:20.

2. Mipango ya maendeleo na usitawi wa watu (Yoeli 2:23). Kwa mfano Mungu anaponyesha mvua ni kwa ajili ya maendeleo na usitawi wa watu, mvua inasababisha watu wapate maji, walime mashamba yao Ili wapate chakula nakadhalika.

3. Mipango ya kueneza ufalme wa Mungu. Hii ni mipango yote ambayo inaufanya ufalme wa Mungu uje au ufike mahali fulani (Mathayo 12:28).

4. Mipango isiyopingana na na neno la Mungu au mipango isiyopingana na mipango ya Mungu. Kwa mfano aliyevuruga mpango wa kujenga mnara wa Babeli ni Mungu kwa kuwa mpango ule ulikuwa kinyume na mipango yake au matakwa yake (Mwanzo 11:1-9).

Chapisha Maoni

0 Maoni