Watu wengi wamekuwa wakibaki nyuma kiuchumi, kiroho, kiheshima, kielimu, kiufahamu nakadhalika bila kujua kinachosababisha hali hiyo ya kubaki nyuma ni roho (Pepo) kutoka kuzimu.
Biblia inatujulisha kisa cha mtu mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka thelathini na nane alikuwa anatamani kupona lakini kila akitaka kuingia mahali ambapo wengine wanapata uponyaji ghafla anakuja mtu mwingine mbele yake halafu yeye anabaki nyuma na anakosa uponyaji, roho ya kubaki nyuma ni mbaya sana, rejea kisa hicho (Yohana 5:1-9).
Jambo mojawapo ambalo Mungu aliwambia wana wa Israeli ni kwamba "hawatakuwa mikia bali watakuwa vichwa" (Kumbukumbu la torati 28:13). Mkia hubaki nyuma, mkia hukaa nyuma.
Mapenzi ya Mungu ni kwamba watu wa Mungu wasiwe nyuma bali wawe mbele kwenye kila eneo (Kumbukumbu la torati 28:13).
Watu wengi wamebaki nyuma sana, kuna wengine unakuta yeye kwao ndiye binti mkubwa lakini wadogo zake wa kike wanaolewa ila yeye anabaki nyuma yao, wengine unakuta yeye tu ndio yuko nyuma kwenye kila kitu kuliko wengine, HIYO NI ROHO YA KUZIMU SIO KAWAIDA - SHITUKA.
Roho ya kubaki nyuma inasababisha ukose nafasi, fursa au vitu ulivyotakiwa kupata wewe "yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ILA WAKATI NINAPOKUJA MIMI, MTU MWINGINE HUSHUKA MBELE YANGU" (Yohana 5:7)
Roho ya kubaki nyuma inasababisha ubaki na wazo au mpango fulani ila kabla haujautekeleza anatokea mtu mwingine kutekeleza "yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ILA WAKATI NINAPOKUJA MIMI, MTU MWINGINE HUSHUKA MBELE YANGU" (Yohana 5:7).
NB: Fukuza roho ya kubaki nyuma itoke kwenye maisha yako kwa jina la Yesu.

0 Maoni