6. Mungu hawezi kukubariki kama hajapata mlango wa kupitishia hizo baraka, Mungu akitaka kukutoa kwenye majaribu, hali ngumu au changamoto fulani huwa anafanya kwanza mlango wa kutokea ili upite (1 Wakorintho 10:13) au Mungu huwa anampa mtu mlango fulani (Ufunuo wa Yohana 3:8) au anaweza kukufungulia mlango fulani (1 Wakorintho 16:9)(2 Wakorintho 2:12).
7. Shetani akitaka kufanya vita au akitaka kukukwamisha huwa anafunga milango ili usipate pa kutokea (Isaya 45:1-3), Yesu alituambia milango ya kuzimu inashindana na kanisa lakini haiwezi kushinda (Mathayo 16:18).
8. Kama milango haijafunguka kuna mambo hayawezi kutokea, kufanyika au kukujia (Isaya 60:11), kama milango haijakufungukia huwezi kufanikiwa kwa lolote, huwezi kupeleka injili sehemu zingine kama milango haijafunguka (Wakolosai 4:3).
MBINU BAADHI ZA KUKUSAIDIA KUMILIKI MALANGO
1. Ifahamu haki yako ya kumiliki malango ya adui zako sawasawa na agano la Mungu kwa Ibrahimu na uzao wake (Mwanzo 22:15-17) kumbuka kuwa kama umezaliwa mara ya pili ndani ya Kristo wewe ni uzao wa Ibrahimu (Wagalatia 3:29).
2. Mtii Mungu, Ibrahimu aliambiwa uzao wake utamiliki mlango wa adui zao baada ya kumtii Mungu (Mwanzo 22:1-17).
3. Maombi, tumia maombi kama njia ya kutumia mamlaka yako ya kutiisha nguvu za giza ambazo zinafunga milango ili usifanikiwe katika jambo lolote, pia tumia maombi kama njia ya kutumia mamlaka yako uliyopewa ndani ya Yesu Kristo kufungua milango iliyofungwa na shetani, Mtume Paulo aliwajulisha Wakolosai kuwa maombi yana mchango katika kufunguka kwa milango mbalimbali (Wakolosai 4:3).

0 Maoni