Kuwahi na kuchelewa yote ni ya muhimu kutegemeana UNAWAHI WAPI NA KWA NINI UNAWAHI NA UNACHELEWA WAPI NA KWA NINI UCHELEWE.
•Kwa mfano mtoto akiwahi kutolewa tumboni kabla ya miezi tisa inaweza kuwa hatari kwake na kwa mama yake pia atatakiwa kupata uangalizi maalumu kwa sababu amewahi kutoka tumboni.
•Kuna wakati kuwahi kuoa au kuolewa ni muhimu na kuna wakati kuchelewa kuoa au kuolewa ni muhimu zaidi kutegemeana na sababu mbalimbali.
•Farasi akimwambia kinyonga unachelewa, si ajabu kinyonga akashangaa kwa kuwa MWENDO NA MAUMBILE YA KINYONGA NI TOFAUTI, kila mtu ana mwendo wake na maumbile yake. Jifunze kuepuka kuendeshwa na maneno ya watu wakuambiao "UNACHELEWA" au "UNAWAHI" usisahau wewe ni wewe na wao ni wao (Kinyonga sio Farasi).
•Kibinadamu, Yesu alichelewa kwenda kumponya Lazaro hatimaye Lazaro akafa lakini kuchelewa kwa Yesu yalikuwa ndio mapenzi ya Mungu (Yohana 11:4-6)
NB: Kuchelewa na kuwahi yote ni ya muhimu kutegemeana unawahi wapi na kwa nini, pia kuna wakati kuchelewa ni muhimu kuliko kuwahi kutegemeana na sababu mbalimbali.

0 Maoni