HALI YA MOYO WAKO INAATHIRI MAISHA YAKO YA MAOMBI


Ninapozungumzia maisha ya maombi nazungumzia utayari wa kumuomba Mungu, jinsi unavyoomba na imani juu ya Mungu unayemuomba. 

Moyo wako ukiathirika, maisha yako ya maombi yanaathirika kwa kiwango kikubwa.

Kwa mfano Nabii Eliya alikata tamaa kabisa, akiwa katika hali ya kukata tamaa angalia kile alichomuomba Mungu, aliomba "MUNGU IONDOE ROHO YANGU KWA KUWA MIMI SIO MWEMA KULIKO BABA ZANGU " 1 Wafalme 19:4

Moyo wa Nabii Eliya ulikwa umeshaathirika, akasahau kuwa MUNGU HUTUTUMIA SIO KWA SABABU SISI NI WEMA KULIKO WENGINE LA HASHA, BALI HUTUTUMIA KUTEGEMEANA NA KUSUDI LAKE MWENYEWE.

Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya moyo wako na maisha yako kwa ujumla ikiwemo maisha yako ya maombi, ndio maana utaona andiko hili liko kwenye Biblia.

"LINDA SANA MOYO WAKO KULIKO YOTE ULINDAYO"

Kama maisha yako ya maombi yameathirika usifanye haraka kukemea pepo wachafu na nguvu za giza, KABLA YA KUKEMEA KAGUA MOYO WAKO.

Je! umebeba uchungu moyoni?

Je! haujasamehe?

Je! unajiona kama panzi kama wale wapelelezi waliotumwa na Musa kule Kanaani?

Je! unahisi Mungu anajali wengine kuliko wewe?

Je! unaona hata bila bila Mungu unaweza kuendelea na safari ya maisha?

Chapisha Maoni

0 Maoni