NENO LA MUNGU KAMA PUMZI


UTANGULIZI

KIla mwanadamu anahitaji pumzi ndio maana wakati Mungu alipomaliza kuumba mtu alimpulizia puani pumzi ya uhai (Mwanzo 2:7)

Wanamichezo wanaoshiriki mchezo wa riadha wanahitaji pumzi ya kutosha Ili wakimbie umbali mrefu, huwezi kukimbia umbali mrefu kama hauna pumzi ya kutosha.

Waimbaji nao wanahitaji pumzi ya kutosha ili waweze kuimba vizuri, waogeleaji nao wanahitaji pumzi ya kutosha ili waweze kuogelea kwa ufanisi.

Kuna wagonjwa huongezewa pumzi (oxygen) wakati wakiendelea na matibabu, pumzi ina nafasi muhimu sana katika kurejesha afya njema.

NENO LA MUNGU KAMA PUMZI

(2 Timotheo 3:16)

Biblia imeweka bayana kuwa neno la Mungu lina pumzi ya Mungu ndani yake kwa hiyo unapoliweka kwa wingi neno la Mungu ndani yako ni sawa na kuongeza kwa wingi pumzi ndani yako.

Pumzi ya Mungu ni ya muhimu kwa kila mtu, pumzi ya Mungu iko kwenye neno la Mungu ukitaka kujiongezea pumzi kwa wingi lazima uhakikishe unajifunza neno la Mungu sana, unalisikia neno la Mungu sana.

Kwa mfano wewe unapozungumza au unapoongea maneno yako huambatana na pumzi yako, neno lolote likikutoka linasukumwa na pumzi iliyoko ndani yako, vivyo hivyo Mungu akiongea pumzi yake huambatana na neno lake ndio maana kila neno la Mungu lina pumzi ya Mungu.

Kwa hiyo mbinu rahisi ya kuongeza pumzi ya Mungu ndani yako ni kujibidiisha katika kujifunza neno la Mungu au kulisikia neno la Mungu.

Chapisha Maoni

0 Maoni