KAZI YA KUWASAFIRISHA WATUMISHI WA MUNGU


 

Zipo kazi nyingi za kufanya katika ufalme wa Mungu, kazi mojawapo ni KUWASAFIRISHA WATUMISHI WA MUNGU kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kazi za Mungu (2 Wakorintho 1:16)(2 Wakorintho 16:6-11)(Tito 3:13)(1 Wakorintho 16:6)(Warumi 15:24)(Warumi 10:15).

Hivyo basi usije ukasingizia wewe sio mwimbaji, sio mhubiri, sio shemasi, sio mzee wa kanisa, sio mwanamuziki, sio fundi mitambo, sio fundi wa rangi, majengo nakadhalika, kazi za kufanya kwenye ufalme ni nyingi sana.

Unaweza kufanya kazi hii ya kusafirisha watumishi wa Mungu kwa kuwalipia watumishi wa Mungu kwenda sehemu mbalimbali, unaweza kununua vyombo vya usafiri kwa ajili ya watumishi wa Mungu ili viwarahisishie utendaji kazi, unaweza kutoa magari yako, meli yako, pikipiki yako, boti yako ili iwasafirishe watumishi wa Mungu kwenda kufanya kazi za Mungu sehemu mbalimbali.

Mungu humbariki atendaye kazi hii.

Chapisha Maoni

0 Maoni