UTANGULIZI
Maombi ni jambo ambalo linapuuzwa na watu wengi kwenye nyakati hizi, suala la maombi halipewi kipaumbele na watu wengi, kama Kuna jambo ambalo halifurahiwi na watu wengi ni maombi, nadhani ni kutokana na shetani kupofusha watu fikira zao kuhusu maombi au kukosa ufahamu Moana kuhusu maombi.
Kama kuna jambo ambalo Yesu alizingatia sana ni maombi (Yesu alikuwa mwombaji) aliomba bila kukoma.
Tunaposoma kwenye Biblia tunagundua kwamba maombi yalisababisha mambo mbalimbali yasitendeke au yasitokee.
BAADHI YA MIFANO KUHUSU NGUVU YA MAOMBI KATIKA KUZUIA MAMBO MBALIMBALI YASITENDEKE AU YASITOKEE
1. Maombi yalizuia Mtume Petro asiuawe, rejea kitabu cha Matendo ya Mitume 12:1-17)
2. Maombi yalizuia Mfalme Hezekia asife, rejea kitabu cha Isaya 38:1-9)
HITIMISHO
Usipuuze maombi kwa kuwa wakati mwingine huwezi kujua maadui wanapanga nini kuhusu wewe, familia yako, kanisa, taifa nakadhalika hata kama unajua yaliyopangwa fahamu kuwa maombi yanaweza kuzuia mambo yaliyopangwa na maadui yasitendeke.
0 Maoni