Mungu aliwaambia Waisraeli nchi wanayoiendea ni nchi ambayo imejaa maziwa na asali, akawaambia kule kuna mataifa saba yenye nguvu kuwashinda nakadhalika.
Walikuwa safarini huku wana picha ya kule wanapokwenda.
Mwaka mpya ni kama nchi ya ugeni ambayo haujawahi kufika, anayeujua mwaka mpya na mambo yake ni Mungu, anayeijua mipango ya shetani katika mwaka mpya ni Mungu tu.
IKO HIVI: Mara nyingi tunapokwenda ugenini huwa tunafikia kwa mwenyeji na kama hatuna mwenyeji huwa tunatafuta mwenyeji ili atuelekeze mazingira ya mahali tulipo.
Mwaka mpya ni nchi ya ugeni, mwenyeji wetu ni Mungu tu anajua mwaka mpya ukoje HIVYO BASI NI VEMA KUMPA MUNGU NAFASI ILI AKUONGOZE.
0 Maoni