WATU USIOTAKIWA KUAMBATANA NAO


Waliokuwa na Yona kwenye safari ya kuelekea Tarshishi walijipata kwenye wakati mgumu, wakapata hasara na wakawa kwenye hatari ya kufikwa na mauti KUTOKANA NA KUAMBATANA NA YONA, Kitabu cha Yona Sura ya kwanza kinaeleza habari hiyo.

Vivyo hivyo kuna watu hujikuta wamepatwa na mambo mabaya kutokana na kuambatana na watu fulani.

Hivyo basi ni muhimu kuwa makini sana na watu wanaokuzunguka au unaoambatana nao katika mambo mbalimbali, ni muhimu kumuhusisha Mungu ili akuondolee watu wasio sahihi kwenye maisha yako, watu usiopaswa kuambatana nao ili uweze kuepuka matatizo yatokanayo na kuambatana na watu wanaoweza kukuathiri.

NB: Yona alipotupwa baharini bahari ikatulia, vivyo hivyo kuna watu ukiendelea kuambatana nao katika mambo mbalimbali hautaepuka matatizo, utaandamwa na matatizo - OMBA MUNGU AKUONDOLEE WATU WASIOTAKIWA KUAMBATANA NA WEWE.

Chapisha Maoni

0 Maoni