BAADHI YA NYENZO MUHIMU KATIKA UONGOZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU

      ✍️ Faraja Gasto

Utangulizi

Kila kiongozi hupenda kuitwa kiongozi mzuri japo si kila kiongozi ni mzuri, ili kiongozi aitwe kiongozi mzuri lazima awe na nyenzo muhimu zitakazomsaidia kuongoza vizuri na kuwasimamia watu vizuri kwa kuwa kuongoza kunahusisha mambo mengi ikiwemo usimamizi wa rasilimali watu (human resource management).

Nyenzo 5 muhimu katika uongozi na usimamizi wa rasilimali watu.

1. Maneno ya kiongozi

Maneno ya kiongozi yana nguvu sana kwa anaowaongoza, maneno ya kiongozi yanaweza kusababisha watu wamkubali kiongozi, wampe ushirikiano nakadhalika, hivyo basi kiongozi anapaswa kuwa mtu mwenye maneno mazuri.

(2 Mambo ya nyakati 32:6-8)

Watu waliguswa na wakahamasika kulipigania taifa lao kutokana na maneno ya Mfalme Hezekia.

(1 Wafalme 12:7)

Mfalme Rehoboamu alipewa ushauri na wazee kuhusu namna gani ataweza kuwaongoza watu vizuri, watu wanaomkubali, jambo mojawapo walilomwambia ni kwamba AWAPE WATU MANENO MAZURI.

2. Maono na malengo ya kiongozi

Kiongozi anapaswa kuwa na picha ya mahali anakowapeleka anaowaongoza pia lazima awe na malengo yanayowagusa anaowaongoza.

(Kutoka 32:7-14)

Musa alikuwa anaowaongoza wana wa Israeli huku akiwa na picha nafsini mwake kuhusu nchi ya Kanaani, aliowaongoza akiwa na lengo la kuwafikisha Kanaani hata ilipotokea Mungu alipotaka kuwafutilia mbali waisraeli, MUSA ALIPINGA MPANGO WA MUNGU WA KUFUTILIA MBALI WAISRAELI KWA KUWA LENGO LAKE ALITAKA AWAFIKISHE KANAANI MAANA NDIO KAZI MUNGU ALIYOMUITIA.

3. Kujali watu

Ni rahisi sana kumuongoza na kumsimamia mtu ambaye anaona unamjali, kujali huwa kunasababisha mtu anakuwa tayari kuongozwa au kusimamiwa.

(Yeremia 29:11)

Mungu kama kiongozi aliwaambia wana wa Israeli "ana mipango mipango mizuri Kwa ajili yao, ni mipango ya kuwapa mema" 

Mungu alikuwa anamaanisha kwamba anawajali sana watu wake ndio maana anawawazia mambo yaliyo mema.

Kujali watu kunahusisha mambo mengi ikiwemo kuwasikiliza watu, ndio maana hata Mungu hutusikiliza tunapomueleza mambo yetu.

4. Tabia ya kiongozi

(1 Wathesalonike 1:5-6)

Jambo mojawapo lililosababisha huduma ya Mtume Paulo na Silwano na Timotheo kukubalika pale Thesalonike ni TABIA ZAO, namna walivyoishi kwa nidhamu ilisababisha watu wakawakubali.

5. Kibali au kukubalika

Kuongoza watu wasiokukubali ni hatari sana kwa kuwa hawatakuwa pamoja na wewe wala hawatakupa ushirikiano, watakuchosha kwa kuwa hawakukubali.

Ni rahisi sana kumuongoza na kumsimamia mtu anayekukubali, hivyo basi kila kiongozi anapaswa kuhakikisha anakubalika kwa anaowaongoza.

Baadhi ya mambo ya kufanya ili ukubalike

a). Hakikisha unakuwa mfano wa kuigwa kwa unaowaongoza.

b). Uadilifu

Hakikisha kile unachosema ndicho unachotenda, hakikisha ndio yako ni ndio na sio ni sio usiwe mtu wa ndio sio.

Hakikisha ukimuahidi mtu jambo unalitimiza.

c). Jali watu, tenda wema kwa watu

d). Heshimu watu 

e). Omba Mungu akupe kukubalika kwa unaowaongoza.

Chapisha Maoni

0 Maoni