Hapa duniani kuna watu wanafahamu siri za aina mbalimbali kama vile siri za wanadamu, siri za serikali nakadhalika.
Kutokana na kufahamu siri hizo ndio maana wanafanikiwa katika mambo yao, ndio maana wanaheshimika, ndio maana wanaogopwa, ndio maana wanalindwa, ndio maana wanajiamini, ndio maana wanashirikishwa katika maamuzi, ndio maana wanapata fedha, ndio maana wanatafutwa ili wauawe nakadhalika. HAYO YANATOKEA KWA SABABU WAMEFAHAMU SIRI FULANI.
IKO HIVI: Mungu anazo siri za aina mbalimbali, Siri mojawapo ya Mungu ni YESU KRISTO yaani Yesu ni siri ya Mungu (Wakolosai 2:2)
Kila ambaye ameifahamu siri hii (aliyemwamini Yesu Kristo) harogwi, anatembea kifua mbele kwa kuwa anajua aliye ndani yake ni mkuu, Mungu anaishi ndani yake na yeye anaishi ndani ya Mungu, ana mamlaka ya juu ya nguvu zote za giza (uchawi, pepo n.k). HAYO YANATOKEA KWA KUWA AMEFAHAMU SIRI YA MUNGU IITWAYO YESU KRISTO.
Hizo ni baadhi ya faida wanazopata wote ambao wamefahamu siri ya Mungu yaani waliomwamini Yesu Kristo.
NB: Ukiifahamu siri ya Mungu (Yesu), pepo (majini) hawatakutesa, ndoto chafu hazitakitesa, mawazo machafu yataachia moyo wako nakadhalika. Kuna watu usiku hawalali kwa sababu hawajafahamu Siri ya Mungu (Yesu), kuna watu wanateswa na pepo (majini) kwa sababu hawajafahamu siri ya Mungu, kuna watu hawana amani kwa kuwa hawajafahamu Siri ya Mungu (Yesu)
Hivyo basi
1. Usiendelee kuteswa na pepo (majini) wakati mlango wa kuijua siri ya Mungu uko wazi.
2. Usiendelee kuteswa na ndoto chafu wakati mlango wa kuijua siri ya Mungu uko wazi.
3. Usiendelee kukosa amani wakati mlango wa kuijua siri ya Mungu uko wazi.
Wito
Kwa yeyote aliye tayari kiufahamu siri ya Mungu wasiliana Nami
WhatsApp +255767955334
Mawasiliano ya kawaida +255625775243
0 Maoni