KIONGOZI MWENYE HURUMA


                    ✍️Faraja Gasto

(Luka 6:36)

Kwa mujibu wa Biblia, sifa mojawapo ya kiongozi mzuri ni HURUMA, yaani kiongozi mzuri ana huruma. Ukifuatilia viongozi wote wabaya sifa mojawapo waliyonayo ni KUTOKUWA NA HURUMA, Kwa tafsiri nyingine ni WAKATILI.

Jifunze kutoka kwenye mifano hii ya baadhi ya viongozi wenye huruma

1. YESU KRISTO (Marko 1:40-42)

Yesu alikuwa kiongozi mwenye huruma sana, yaani alipoona mtu ana tatizo alimuhurumia akatatua tatizo lile.

Siku fulani Yesu alikwenda kutembelea kwa Mtume Petro akamkuta mama mkwe wa Petro akiwa mgonjwa, Yesu akamuhurumia akamponya (Mathayo 8:14-15)

Siku fulani Yesu alikutana na msafara unakwenda kuzika, alipomtazama mama wa mtoto aliyekufa, Yesu alimuonea huruma akamfufua yule kijana (Luka 7:11-15)

2. MUSA (Kutoka 32:9-15)

Kama taifa la Israeli lipo katika dunia hii ni kwa sababu ya kiongozi mwenye huruma aliyeitwa Musa, Mungu aliwahi kutaka kulifutilia mbali taifa la Israeli lakini Musa akawaonea huruma watu wale kisha akawaombea Kwa Mungu asiwafutilie mbali.

3. NABII SAMWELI (1 Samweli 16:1)

Mungu alipomkataa Mfalme Sauli, Nabii Samweli alimuombea sana Kwa Mungu japo Mungu alikataa maombi ya Samweli, kilichokuwa kinamsukuma Nabii Samweli kuomba ni huruma, alimuonea huruma Sauli.

UTAJUAJE MTU AU KIONGOZI ANA HURUMA?

1. Anajali matatizo ya watu au anajali maumivu ya wengine.

(Luka 7:11-15)

Kilio cha mjane aliyekuwa akimlilia mtoto wake aliyekufa kilimfanya Yesu amuonee huruma, ilibidi Yesu amfufue yule kijana. Mtu mwenye huruma au kiongozi mwenye huruma anajali maumivu ya wengine.

(Luka 10:30-35)

Msamaria mmoja mwenye huruma alihakikisha mtu aliyevamiwa na kujeruhiwa na majambazi anapata matibabu na aanarejea katika afya njema, Biblia haituambii kwamba huyu Msamaria na yule jamaa aliyejeruhiwa na majambazi walikuwa wanafahamiana ila Biblia inatuambia yule Msamaria alimjali yule jamaa Kwa kuwa alimwonea huruma.

2. Anawaombea watu kwa Mungu.

(Kutoka 32:9-15)

Musa alipowahurumia wana wa Israeli aliwaombea Kwa Mungu ili asiwaangamize.

(1 Samweli 16:1)

Mungu alipomkataa Mfalme Sauli, Nabii Samweli alimuombea sana Kwa Mungu japo Mungu alikataa maombi ya Samweli, kilichokuwa kinamsukuma Nabii Samweli kuomba ni huruma, alimuonea huruma Sauli.


3. Hafurahii kuona watu wakipatwa na mabaya.

(Yeremia 29:11)

Mungu kama kiongozi mwenye huruma aliwahi kuwaambia wana wa Israeli kuwa yeye ni Mungu anayewawazia mema wala si mabaya kwa kuwa hafurahii kuona wakipatwa na mabaya. Hata sasa bado Mungu ana huruma kutokana na huruma zake hafurahii kuona watu wakipatwa na mabaya 

MTU AU KIONGOZI ASIYE NA HURUMA ANA SIFA ZIFUATAZO

Baadhi ya sifa ni

1. Hajali watu 

2. Haombei watu

3. Mtu au watu wakipatwa na mabaya haimsumbui 




Chapisha Maoni

0 Maoni