Na:Mwl.Faraja Gasto
Bwana Yesu Asifiwe.
Tunaishi katika dunia ambayo imejaa uasi na ubaya wa kila namna, kutokana na ubaya uliomo duniani kila mwanadamu hujikuta akiwa ana maadui, hata maadui zako nao wana maadui zao.
Kutokana na uadui huo, maadui hupanga mipango mbalimbali ya kumshambulia mtu lakini kwa kuwa Mungu ameahidi kuwalinda watu wake (Isaya 54:17) Mungu huwa anampa mtu taarifa kuhusu shambulizi lililokusudiwa juu yake kabla shambulizi hilo halijatokea.
N:B watu wengi wamejikuta kwenye mitego na mateso kutoka kwa madui zao kwa kuwa WALIPUUZIA TAARIFA ZA TAHADHARI walizopewa na Mungu kuhusu mipango mibaya inayopangwa na adui.
Usisahau hili "Hakuna shambulizi litakupata kabla Mungu hajakupa taarifa"

NJIA AMBAZO MUNGU ANAZITUMIA KUMPA MTU TAAARIFA
1.Njia Ya Ndoto
Soma Ushuhuda Wangu Mwenyewe.
Siku Moja niliota nilikuwa napita mahali fulani nikakuta katika lile eneo kuna ugomvi kati ya rafiki yangu na mtu fulani sikumjua, Nilipofika nikaanza kuwaamua lakini yule rafiki yangu akampiga yule mtu hatimaye akafa ghafla wakatokea maaskari walipouliza nani kaua, yule rafiki yangu akasema ni mimi nimeua ikabidi nikamatwe na wale maaskari. Baada ya kukamatwa nilishtuka kutoka usingizini lakini moyo wangu ulikosa amani kabisa nikahisi nimekamatwa kabisa.
Nilichofanya nilienda kuombea ili kukataa huo mpango wa maadui wa kunibambikizia kesi, nilipoomba namna hiyo hiyo ghafla amani ikarudi moyoni na nikajua tayari hiyo vita Bwana amenishindia.
Ninachotaka ufahamu ni kwamba Mungu huwa anampa mtu taarifa kwa njia hii ya ndoto kuhusu mipango mibaya dhidi yake ili mtu achukue hatua ili asiingie kwenye hali wamtakiayo adui zake.

(Mwanzo 40:7-19)
Tunaona watu wawili walipewa taarifa na Mungu kuhusu mipango inayopangwa dhidi yao, mmoja akaambiwa BAADA YA SIKU 3 ATAUAWA lakini hatuoni akichukua hatua zozote ili asije akauawa, na mwishowe alikufa. Huyo Jamaa alipata tafsiri ya ndoto lakini tafsiri haikumsaidia kuepuka mauti iliyokuwa mbele yake, Kwa hiyo ni vema ufahamu kuwa hata ukipata tafsiri ya ndoto na ukaacha kuchukua hatua stahiki utajikuta unasema "ILA HILI TUKIO NILILIOTA". Kwani hujawahi kuona mtu anaota mtu fulani kafariki halafu baada ya muda kweli huyo mtu anasema "Ila niliota", mimi nakuambia shida sio kuota ndoto ila je! Baada ya kuota ndoto za namna hiyo unachukua hatua gani?

Waweza kumshirikisha mwingine, Barikiwa.
0 Maoni