KWA NINI HUTAKIWI KUOGOPA KUCHUKUA HATUA ZA HATARI

©Faraja Gasto

Hutakiwi kuogopa kuchukua hatua za hatari kwa sababu kuna wakati Mungu huwa anaweka WAZO LA KUCHUKUA HATUA ZA HATARI NDANI YA MTU ili mtu huyo akichukua hatua za hatari kusudi la Mungu lisimame kwenye maisha yake n.k

Ngoja nikupe mifano hii miwili ili unielewe

1. YONA 1:8-17
Ukisoma habari za Nabii Yona utaona alipokataa kwenda Ninawi Mungu alichafua bahari na akaaandaa samaki ambaye atammeza Yona ili ampeleke Ninawi, Wakati Yona akiwa kwenye mashua alijikuta amepata WAZO LA KUTUPWA BAHARINI unaweza ukadhani Yona alitaka kufa baharini lakini hilo wazo la kutupwa Baharini ni Mungu aliliweka ndani ya Yona kwa sababu Mungu aliandaa samaki pale baharini ili ammeze Yona na kumpeleka Ninawi. Baada ya siku tatu Yona anakuja kujikuta yuko Ninawi ikabidi afanye kazi aliyotumwa na Mungu.

2. 2 WAFALME 7:1-8
Ukisoma utaona Nabii Elisha akitoa unabii kuhusu upatikanaji wa chakula, baada ya hapo Mungu aliweka WAZO LA KUCHUKUA HATUA ZA HATARI ndani ya wakoma waliokuwa nje ya mji. Wakoma walisema hivi "kama tukifa acha tufe" lakini ni bora tufe tukiwa tumechukua hatua.
--Hilo wazo la kujitoa mhanga ni Mungu aliliweka ndani yao ili wafanyike ukombozi kwa taifa na hatimaye unabii wa Elisha utimie.
KWA HIYO
Si kila wazo la kuchukua hatua za hatari huwa linatoka kwa shetani, mawazo mengine ya kuchukua hatua za hatari huwa yanatoka kwa Mungu na unapochukua hatua utaona mbingu zinasimama na wewe.
Barikiwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni