Mwl. Faraja Gasto
Bwana Yesu Asifiwe,
Katika Sehemu ya kwanza nilifundisha kuwa Mingu anatumia njia ya ndoto.
Leo naendelea na njia ya pili ambayo Mungu anaitumia kumpa mtu taarifa kuhusu shambulizi au mipango mibaya iliyopangwa dhidi yake.

2.Njia Ya Pili: Mungu Ataufunua moyo wa mtu anayekuwazia mabaya KUPITIA USO WAKE
(Mwanzo 31:1-5)
Ukisoma kitabu cha Mwanzo 29:19-30) utaona Labani mjomba wake yakobo alikuwa anatamani Yakobo awe mtumwa wake siku zote, ilifika hatua USO WA LABANI ukambadilikia Yakobo (Mwanzo 31:1-5)Hiyo ilikuwa ishara kuwa anachokusudia Labani sio kizuri.
Mungu huwa anampatia mtu taarifa kuhusu mipango mibaya dhidi yake kwa kufunua mioyo ya waliompangia mtu mabaya KUPITIA NYUSO ZAO, ukianza kuona USO WA MTU UNAKUBADILIKIA tofauti na jana na juzi, ni vema ujue unapewa taarifa kuna shambulizi au mpango mbaya dhidi yako kwa hiyo ni muhimu kuchukua tahadhari kwa kumsikiliza Mungu atakupa maelekezo gani ili ushinde hiyo vita.
Mungu akubariki, mshirikishe mwingine maarifa haya
Zidi kufuatilia......................

0 Maoni