Faraja Gasto
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo.
Nahitaji kwenda moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu
-->Kosa ambalo linafanywa na viongozi wa makanisa ni KUWEKA JUHUDI KUTENGENEZA WAUMINI kuliko KUTENGENEZA WANAFUNZI.
--->Kuna tofauti kati ya MUUMINI na MWANAFUNZI, kanisa la sasa lina waumini wengi na lina wanafunzi wachache.
-->Ni vema kila mtu aelewe kuwa Bwana Yesu hakutuagiza kuwafanya watu kuwa waumini bali alituagiza kuwafanya watu kuwa wanafunzi.
--->Waumini ni wale ambao wanakuja kanisani kwa msukumo wa hisia kwa mfano wanaokuja kanisani kuangalia na kusikiliza jinsi waimbaji wanavyoimba, na ikitokea siku hiyo waimbaji wakaimba kidogo basi waumini wataondoka wamekwazika na pia ikitokea muhubiri akahubiri kupita muda waliouzoea basi wataondoka wamekwazik, pia waumini ni watu ambao hawako tayari kuitoa miili yao kuwa dhabihu takatifu kwa Mungu wao n.k(HAO NDIO WAUMINI)
Lakini WANAFUNZI ni wale watu ambao kiu yao kubwa ni kujifunza kutoka kwa Bwana wao Yesu kila iitwapo leo, hawa ndio watu wamjuao Mungu wao kwa hiyo hawawezi kufuata upepo wowote unaoletwa na adui, wanafunzi huwa wanaisikia sauti ya Mchungaji wao(Yesu) kwa kuwa wanaijua n.k
MADHARA YA KUWA NA WAUMINI WENGI MAKANISANI BADALA YA KUWA NA WANAFUNZI WENGI
KATIKA JAMII
1.Waumini huwa hawana ushuhuda mzuri(matendo yao hayamuwakilishi Yesu)
2.Waumini huwa hawajulikani kama wameokoka au hawajaokoka kwa kuwa hawana tofauti na ambao hawajaokoka.
KATIKA NGAZI YA TAIFA
1.Taifa linakosa watu waaminifu wa kusimamia mambo mbalimbali kwa uwazi na ukweli.
2.Rasilimali za nchi zinatumiwa vibaya na wakati mwingine zinauzwa kienyeji kwa nchi jirani.
-->Kumbuka kuna viongozi ambao ni washirika wa makanisa mbalimbali ila kwa kuwa hawaandaliwi kuwa wanafunzi wa Yesu basi kula rushwa na kuishi maisha ya ufisadi kwao ni kawaida.
(HAYO NI BAADHI YA MADHARA YATOKANAYO NA KUWAFANYA WATU KUWA WAUMINI BADALA YA KUWAFANYA KUWA WANAFUNZI)
N.B Ni wakati sahihi wa kurudi kwenye agizo kuu la Yesu.
Barikiwa.
0 Maoni